IQNA

Mchujo katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani

13:53 - January 08, 2022
Habari ID: 3474780
TEHRAN (IQNA) – Duru ya mchujo ya Mashindano ya 38 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Iran imepangwa kuanzia Januari 9 mjini Tehran.

Kwa mujibu wa taarifa mashindano hayo ambayo yanafanyika kwa njia ya intaneti katika duru hii yataandaliwa katika Ukumbi wa Basirat kuanzia Januari 9-10 kitengo cha wanawake na mashidano ya wanaume yatafanyika kuanzia Januari 12 hadi 15.

Akizungumza mwezi Oktoba mwaka 2021, Mehdi Ghare-Sheikhlou, mkuu wa masuala ya Qur'ani katika Shirika la Wakfu la Iran alisema nchi 53 zilikuwa zimeshawasilisha majina ya wawakilishi wao katika mashindano hayo.

Akizungumza katika mahojiano na Televisehni ya Qur'ani ya Iran, afisa huyo amesema mashindano hayo ya kimataifa yatakuwa na vitengo vine vya wanaume, wanawake, wanafunzi wa shule na wenye ulemavu wa macho.

Halikadhalika alibaini kuwa duru ya mchujo ya mashindano hayo itafanyika kwa njia ya intaneti ambapo watakaofaulu watashiriki fainali katika mashindano yatakayofanyika nchini Iran baadaye mwezi Machi mwaka huu na hilo litategemea hali ya janga la COVID-19 duniani.

Shirika la Wakfu la Iran huandaa mashhindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Iran ambapo washindani kutoka kila kona ya dunia hushiriki.

5394497

captcha