IQNA

Ramadhani katika ardhi ya Wahyi

TEHRAN (IQNA) - Msikiti Mkuu wa Makka (Masjid al-Haram) mjini Makka na Msikiti wa Mtume SAW (Al-Masjid an-Nabawī) huko Madina huwa na mamia ya maelfu ya waumini wakiwemo wanaoshiriki katika Hija ndogo ya Umrah ktika mwezi mtukufu wa Ramadhani kila mwaka.

Kusali Sala ya jamaa na kushiriki katika Futari ni kati ya nukta muhimu za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na ni miongoni mwa madhihirisho matukufu ya umoja wa Kiislamu na kumtumikia Mwenyezi Mungu miongoni mwa Waislamu.