IQNA

Umrah

Wanaoshiriki Umrah wapokea nakala za Qur'ani ndani ya Ramadhani

22:27 - April 05, 2023
Habari ID: 3476817
TEHRAN (IQNA) - Katika siku 10 za mwanzo za mwezi uliobarikiwa wa Ramadhani zaidi ya nakala 30,000 za Qur'ani zilisambazwa miongoni mwa Waislamu wanaoshiriki kaktika Hija Ndogo ya Umrah na wageni wa Msikiti Mkuu wa Makka, Al Masjid Al Haram a, na Msikiti wa Mtume SAW, Al-Masjid an-Nabawi,.

Ofisi ya Urais Mkuu wa Masuala ya Msikiti Mkuu na Msikiti wa Mtume, ikiwakilishwa na Utawala Mkuu wa Masuala ya Qur'ani Tukufu, ilitangaza takwimu hizo, Shirika la Habari la Saudia liliripoti Jumanne.

Mkurugenzi wa Idara ya Masuala ya Qur'ani Tukufu Saudia Saad bin Ghuwailib Al-Nadawi alisema kuwa zawadi ya nakala Misahafu ni moja ya zawadi muhimu zaidi kati ya zile zinazotolewa kwa wageni na Ofisi ya Rais Mkuu wa Masuala ya Msikiti Mkuu na Msikiti wa Mtume.

Siku ya Jumatatu, ilitangazwa kuwa mamilioni ya mahujaji wa Umrah, waumini na wageni wa Msikiti Mkuu wamehudumiwa wakati wa theluthi ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

3483078

Kishikizo: umrah qurani tukufu
captcha