IQNA

Makka na Madina

Waumini wajaa katika Msikiti Mkuu na Msikiti wa Mtume SAW katika Usiku wa Qadr

20:36 - April 18, 2023
Habari ID: 3476885
TEHRAN (IQNA) - Mnamo usiku wa 27 wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, unaoaminika kuwa Usiku wa Qadr, mamilioni ya waumini walijaa Msikiti Mkuu ya Makka (Masjid al Haram) na Msikiti wa Mtume SAW (Masjid An Nabawi) huko Madina.

Mamlaka zimekuwa zikisimamia wimbi la waumini waliofika  kwenye misikiti hiyo miwili mitakatifu wakati wa mwezi wa Ramadhani, mojawapo ya nyakati zenye shughuli nyingi zaidi za mwaka.

Zaidi ya wageni milioni moja walikuwepo kwenye Msikiti Mkuu wa Makka siku ya Jumapili.

Urais Mkuu wa Masuala ya Msikiti Mkuu na Msikiti wa Mtume (saww) alisema kulikuwa na wafanyakazi 4,000 kwenye Msikiti Mkuu na kwamba msikiti huo ulikuwa ukisafishwa usiku na mchana na timu 70 za wahudumu.

Mpango mpya ulizinduliwa katika Msikiti Mkuu ili kuboresha huduma kwa wageni wakiwemo wazee na walemavu.

Mradi huo ni sehemu ya kampeni ya “Ni Heshima Kuwahudumia Mahujaji Wetu” ambayo inaonekana kuhakikisha waumini wanapata huduma bora zaidi kuanzia wanapowasili hadi wanapoondoka. Aghalabu ya waumini wanaofika Makka wakati huu hutekelelza ibada ya Hija ndogo ya Umrah

Mkuu wa ofisi ya rais, Abdulrahman Al-Sudais, aliongoza waumini katika sala za usiku mjini Makka.

3483253

captcha