IQNA

Mawaidha

Fadhila za Ijumaa za Ramadhani

15:58 - April 06, 2023
Habari ID: 3476822
TEHRAN (IQNA) – Katika utamaduni wa Kiislamu, Ijumaa ni maalum kwa ajili ya ibada na kujumuika familia. Wakati huo huo, Ijumaa huwa muhimu zaidi katika mwezi uliobarikiwa wa Ramadhani kwa sababu mwezi huu ni bora kuliko nyakati zingine zote.

Kitabu "Kanz al-Maram fi Amal Shahr al-Siyam" kimeashiria baadhi ya matendo yaliyopendekezwa kwa siku hizi.

Kwa mujibu wa riwaya, usiku na siku za Ijumaa ni bora kuliko Ijumaa za miezi mingine.

Imam Baqir (AS), Imam wa tano wa Waislamu wa madhehebu ya Shia, alikuwa akienda msikitini mapema Ijumaa ya Ramadhani, akisema: "Ubora wa Ijumaa ya Ramadhani ikilinganishwa na jumaa ya miezi mingine ni kama ubora wa Ramadhani ikilinganishwa na miezi mingine."

Vile vile aliufaninisha ubora huu kama ubora wa Mtume Muhammad (SAW) ikilinganishwa na mitume wengine.

Jambo bora katika Ijumaa ya Ramadhani

Mtume Muhammad (SAW) amenukuliwa akipendekeza Waislamu kuwasomea Salawat Ahlul-Bayt siku ya Ijumaa ya Ramadhani.

Matendo kama vile usomaji wa Qur'ani Tukufu, Ghusl, n.k. ambayo yamependekezwa siku ya Ijumaa yanapata thawabu zaidi katika Ijumaa za Ramadhani.

Kwa mujibu wa Allamah Majlisi, Imam Sajjad (AS) alikuwa akitoa khutba za Ijumaa za Ramadhani kwa watu wa Madina.

Katika moja ya khutba, alionya watu dhidi ya kumsahau Mwenyezi Mungu na kifo. "Kifo kiko karibu na wewe kuliko kitu kingine chochote," alisema, akiwahimiza watu kufikiria wakati wa kuwekwa ndani ya makaburi yao.

Akizungumzia maswali yatakayoulizwa kutoka kwa wafu na Malaika, Imam Sajjad alisema: “Kitu cha kwanza watakachouliza ni kuhusu Mwenyezi Mungu mliokuwa mnamuabudu, kisha watamuuliza Mtume aliyetumwa kwenu, dini mliyoifuata, kitabu ulichosoma, Imamu uliyempenda na kumfuata, maisha na mali yako.”

Alitoa wito kwa watu kujiandaa kwa maswali haya kwa kuchunga matendo yao katika ulimwengu huu.

Kishikizo: ijumaa ramadhani fadhila
captcha