Hafla hiyo pia ilitumika kama kumbukumbu ya hayati Rais wa Iran Shahidi Ebrahim Raisi, huku washindani na umati wa waliohudhuria wakitoa heshima.
Tukio hilo lilifanyika wakati Iran ikiomboleza vifo vya kusikitisha vya Rais wa Iran Ebrahim Raisi, Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollahian, na ujumbe walioandamana nao katika ajali ya helikopta kaskazini magharibi mwa nchi siku ya Jumapili. Iran iko katika siku tano za maombolezo, huku shughuli za kuwaaga mashahidi zikianza leo.