IQNA

Maombolezo

Haram ya Imam Ridha (AS) , mahali alipozikwa Shahidi Rais Raisi

18:23 - May 24, 2024
Habari ID: 3478878
IQNA - Hayati rais wa Iran shahidi Ebrahim Raisi amezikwa katika Haram Takatifu ya Imam Ridha (AS) huko Mashhad kaskazini mashariki mwa Iran na hivyo kuashirikia mwisho wa hafla za kuuaga wake na  mashahidi wenzake zilizohudhuriwa na mamilioni ya waombolezaji Wairani katika katika miji kadhaa.

Takriban waombolezaji milioni tatu walifika  katika mji aliozaliwa wa Mashhad siku yaAlhamisi kumuaga Rais Raisi, meya wa jiji hilo kubwa alisema, kufuatia hafla za kumuaga yeye na wenzake katika miji ya Tabriz, Qom, Tehran na Birjand.

Baadaye jioni, mwili wa rais ulishushwa ndani ya kaburi kwenye Haram ya Imam Ridha (AS), ambapo imamu wa nane wa Waislamu wa madhehebu ya Shia amezikwa. Mamilioni ya wafanyaziayar huzuru eneo hilo takatifu kila mwaka.

Rais huyo aliyekuwa na umri wa miaka 63 alipoteza maisha siku ya Jumapili akiwa na waziri wake wa mambo ya nje na wengine sita baada ya helikopta yao kuanguka katika eneo lenye milima kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo wakati wakielekea kuzindua kitengo kilichoboreshwa cha kusafisha mafuta huko Tabriz.

Tukio hilo liliikumba Iran kwa mshtuko na kulitumbukiza taifa katika majonzi  na mshikamano kutoka kwa Waislamu na wasio Waislamu duniani kote.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei, akielezea masikitiko yake makubwa juu ya kifo cha shahidi Raisi na wenzake, alitangaza siku tano za maombolezo ya kitaifa siku ya Jumatatu.

Trela  lililobeba majeneza ya mashahidi lilivutia idadi kubwa ya waombolezaji ambao walijaa kwenye barabara kuu kwa kilomita kadhaa, popote ilipoenda. 

Mjini Tehran, Ayatullah Khamenei aliongoza sala ya Maiti ya mashahidi siku ya Jumatano jijini Tehran katika ibada iliyohudhuriwa na mamilioni wakiwemo wawakilishi wa makundi ya muqawama. Baada ya swala kabla ya mamilioni ya watu waliandamana na  msafara wa majeneza hadi medani ya Azadi jijini  Tehran.

"Ee Mwenyezi Mungu, hatukuona chochote isipokuwa kizuri kutoka kwake," Ayatullah Khamenei alisema wakati wa Swala kwa Kiarabu. Kaimu rais wa Iran, Mohammad Mokhber, na maafisa wengine walisimama karibu naye huku wengine wakishindwa kujizuia na kulia waziwazi.

Kiongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, Ismail Haniyah alihudhuria ibada hiyo ya kumswalia shahidi Rais Raisi na wenzake na akahutubia hadhirina na kusemba kwamba Operesheni ya Kimbuga cha Al Aqsa mnamo Oktoba 7 ya wapiganaji wa Palestina dhidi ya Israeli ilikuwa "tetemeko la ardhi katika moyo wa taasisi ya Kizayuni".

Mwishoni mwa Jumatano, viongozi wa muqawama kutoka Palestina, Lebanon, na Yemen  walikutana kando ya mazishi na Jenerali Hossein Salami, kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, na Esmail Qa'ani, mkuu wa Kikosi cha Quds cha jeshi hilo, kwa mazungumzo juu ya vita vinavyoendelea vya Israel huko Gaza.

Wawakilishi kutoka Asia Magharibi, Afrika Kaskazini na kwingineko kutoka baadhi ya nchi 60 walihudhuria ibada ya kumbukumbu ya baadaye, akiwemo Waziri Mkuu wa Iraq Mohammed Shia' al-Sudani, Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif, Emir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani na Rais wa Tunisia Kais Saied.

Rais wa Tajikistan Imomali Rahmon, Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan, Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Prince Faisal bin Farhan na Sheikh Abdullah bin Zayed, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa UAE, walikuwa wawakilishi wengine waliosafiri hadi Tehran, kukutana na viongozi wa Iran kuelezea rambirambi zao.

Siku ya Alhamisi, mamilioni ya wanaume na wanawake waliovalia mavazi meusi walikusanyika karibu na Haram ya Imam Ridha (AS) chini ya kuba lake la dhahabu katika maombolezo.

Baadhi wakiwa wameshika maua meupe, huku wengine wakiwa na mabango ya juu ya kumuenzi Rais Raisi kama "mtu wa uwanja wa mapambano" wakati lori kubwa lililobeba mwili wake likipita kwenye bahari ya waombolezaji.

"Nimekuja, Ewe Shah, Nipe Hifadhi," ilisema maandishi makubwa ya Kifarsi yaliyoandikwa juu ya lori, yakimuashiria Imam Ridha (AS).

Mabango ya Rais Raisi, bendera nyeusi na alama za kidini ziliwekwa kando ya mitaa ya Mashhad, haswa karibu na mahali pake pa kupumzika.

Hapo awali makumi ya maelfu ya watu walijipanga katika mitaa ya Birjand, mji mkuu wa mkoa wa mashariki wa Khorasan Kusini, kumuaga marehemu rais wakati jeneza lake likipita kwenye barabara kuu.

Rais Raisi alikuwa mwakilishi wa Khorasan Kusini katika Baraza la Wanazuoni Wataalamu ambalo lina jukumu la kumchagua na kusimamia kazi za Kiongozi Muadhamu wa Iran.

3488470

Habari zinazohusiana
captcha