IQNA

Maombolezo

Waislamu Tanzania washiriki katika maombolezo ya shahidi Rais Ebrahim Raisi na wenzake

11:04 - May 25, 2024
Habari ID: 3478883
IQNA-Waislamu nchini Tanzania wameshiriki katika kikao cha kumuomboleza na kumuenzi Shahidi Ebrahim Raisi, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliyekufa shahidi Jumapili iliyopita katika ajali ya helikopta akiwa na wenzake akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollahian.

Kwa mujibu wa taarifa,  Waislamu wa Tanzania wamefanya kumbukumbu ya maombolezo ya kumuenzi Rais wa Iran aliyeaga dunia Ebrahim Rais pamoja na maafisa wengine aliokuwa ameambatana nao akiwemo waziri wake wa mashauri ya kigeni Hussein Amir-Abdollahian.

Maombolezo hayo yaliyoambatana na khitma ya Qur'ani Tukufu kwa ajili ya mashahidi hao yamefanyika katika Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Dar es Salaam.

Washiriki wa kumbukumbu hiyo mjini Dar es Salaam wamemtaja shahidi Ebrahim Rais kwamba, hakuwa Rais wa Iran tu bali alikuwa mwakiilishi wa watu wote wanaodhulumiwa duniani.

Wazungumzaji katika hafla hiyo wamemtaja Ebrahim Raisi kama mwanasiasa aliyekuwa na misimamo thabiti ambaye hakusita kutetea haki na alikuwa mstari wa mbele kutetea taifa madhulumu la Palestina.

Hafla hiyo iliyoongozwa na mwambata wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania Dr. Mohsen Maarefi ilihudhuriwa na shakhsia na viongozi mbalimbali wa dini ya Kiislamu nchini humo.

Rambirambi za Rais Samia

Wakati huo huo Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameungana na viongozi wa mataifa mengine duniani kumuomboleza Ebrahim Raisi wa Iran.

Rais Samia aungana na viongozi wa mataifa mengine kumuomboleza Ebrahim Raisi

Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mara nyingine tena ametoa mkono wa pole kwa wananchi wa Iran kutokana na kuondokewa na kiongozi wao Rais Ebrahim Raisi aliyeaga dunia Jumapili iliyopita katika ajali ya helikopta.

Rais Samia Suluhu Hassan jana alikwenda katika ubalozi wa Iran mjini Dar es Salaam na kusaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi huo kufuatia Kifo cha Rais wa nchi hiyo Hayati Ebrahim Raisi.

Rais Samia alitumia fursa hiyo pia kumpa pole balozi Hossein Alvandi Bahineh pamoja na maafisa mbalimbali wa ubalozi huo na kueleza kuwa, taifa la Tanzania lipo pamoja na Iran katika kipindi hiki kigumu cha msiba mkubwa.

Helikopta iliyokuwa imembeba Sayyid Ebrahim Raisi, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Jumapili jioni Mei 19, 2024 ilipata ajali ilipokuwa ikirejea kutoka kwenye hafla ya ufunguzi wa bwawa la Qiz Qalasi kwenye mpaka wa pamoja wa Iran na Jamhuri ya Azerbaijan.  

4217962

 

Habari zinazohusiana
captcha