Qur’ani Tukufu inasema katika Aya ya 100 ya Surah An-Nisa: “Na mwenye kuhama katika Njia ya Mwenyezi Mungu atapata pengi duniani pa kukimbilia, na atapata wasaa. Na anaye toka nyumbani kwake kuhama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kisha yakamfika mauti njiani basi umethibiti ujira wake kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye maghfira na Mwenye kurehemu.”
Kuhama kwa njia Mwenyezi Mungu na Mtume (SAW), kwa mujibu wa aya hii, kunaweza kufasiriwa kama kuhamia katika ardhi ya Uislamu. Lakini pia inaweza kumaanisha uhamaji wowote kwa lengo la kupata ridhaa ya Mwenyezi Mungu na kutimiza Wajib (kitendo cha faradhi).
Kwa mfano, mtu anayetoka nyumbani kwenda Kuhiji, au kuhudumia watu au hata kuandaa chakula cha kulisha familia yake, anaweza kuwa mfano wa kuhama huko.
Maneno “umethibiti ujira wake kwa Mwenyezi Mungu” yaonyesha kwamba hakika itakuwa thawabu kubwa. Aya haizungumzii baraka kama vile pepo bali malipo ambayo yatatolewa tu na Mungu. Sentensi ya mwisho, “Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu,” ni msisitizo juu ya ukweli kwamba ahadi ya kutoa thawabu kama hiyo itatimizwa kwa hakika.
Yaliyomo katika aya hiyo si kwa ajili ya watu walioishi wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (SAW) bali ni ya kweli kwa zama zote, ingawa Sha'an Nuzul (sababu ya kuteremshwa) ya Aya hiyo ilihusiana na hali ya Waislamu wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (SAW) na katika kipindi cha kati ya kuhama kwao Madina na Kutekwa kwa Makka.
3488421