IQNA

Hotuba

Nasrallah: Shahidi Raisi alikuwa na imani thabiti kuhusu harakati ya ukombozi wa Palestina

10:47 - May 25, 2024
Habari ID: 3478882
IQNA – Kiongozi wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema rais wa Iran hayati Ebrahim Raisi alikuwa na "imani  imara" kuhusu kadhia ya mapambano ya ukombozi wa Palestina.

Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrallah aliyasema hayo katika hotuba yake aliyoitoa katika mji mkuu wa Lebanon Beirut katika khitma ya Shahidi Raisi na wenzake waliouawa shahidi katika ajali ya helikopta kaskazini magharibi mwa Iran siku ya Jumapili.

Nasrallah pia amemtaja Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian, ambaye pia aliuawa shahidi katika tukio hilo, kuwa ni "muumini wa muqawama na harakati zake."

Kiongozi huyo wa Hizbullah amelitaja tukio hilo la ajali  kuwa ni la kusikitisha sana nchini Iran na kimataifa.

Amebainisha kuwa mazishi ya mashahidi hao yalihudhuriwa na mamilioni ya watu katika Jamhuri ya Kiislamu. "Misafara ya mazishi iliyo ni ya tatu kwa ukubwa katika historia ya wanadamu baada ya ile ya mazishi ya Imam Khomeini na Shahidi Qassem Soleimani."

Hapo alikuwa akiashiria a marehemu muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu na kamanda wa zamani wa Kikosi cha Walinzi wa Kikosi cha Quds cha Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (RGC).

Mahudhurio hayo makubwa, alisema, yalikuwa ni ushahidi wa "uaminifu, utiifu, na dhamira thabiti ya watu wa Iran kwa njia ya Imam Khomeini na kwa uongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran."

Janga hilo, hata hivyo, halijaidhoofisha nchi wala "kulitikisa" mkuu huyo wa Hizbullah , alisongeza na kusema kuwa Iran inasalia kuwa muungaji mkono mkuu wa kadhia ya Palestina ya ukombozi kutoka kwa uvamizi na ukoloni  wa Israel.

Kwingineko katika matamshi yake, Nasrallah ameashiria vita vilivyoanza mwezi wa Oktoba ambavyo utawala wa Israel umekuwa ukiviendesha dhidi ya Ukanda wa Gaza kufuatia Operesheni ya Kimbunga cha Al Aqsa, ambayo  ilitekelezwa na wapigania ukombozi wa Palestina ili kulipiza kisasi jinai za miongo kadhaa za Israel dhidi ya Wapalestina.

"Adui anakubali  masaibu makali anayokabiliana nayo na anakubali kutokuwa na uwezo na pia kushindwa kwake," alisema.

Mkuu huyo wa Hizbullah alikuwa akimaanisha kushindwa kwa Tel Aviv hadi sasa kufikia malengo ambayo huko Gaza ikiwa ni pamoja na kushindwa kusambaratisha harakati za wapigania ukombozi wa Palestina na pia kushindwa kuwaokoa mateka Wazayuni wanaoshikiliwa Gaza.

"Leo, tukiwa katika mwezi wa nane wa vita dhidi ya Gaza, Waisraeli wenyewe, walio madarakani na wapinzani, wote wanakubali kwamba kile ambacho chombo hicho kimepata mwaka huu hakina kifani," Nasrallah alisema.

Alibainisha ombi la hivi karibuni la Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) Karim Khan la kutaka kukamatwa kwa wahalifu wa kivita wa Israel akiwemo Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kutokana na ukatili wao huko Gaza.

"Nani angeamini kwamba wakati ungefika ambapo Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ingeomba kutolewa kwa hati za kukamatwa kwa maafisa wa Kizayuni, na hii ni moja ya matokeo ya Kimbunga cha Al-Aqsa," kiongozi wa Hizbullah alisema.

Vile vile amesisitiza kuwa iwapo utawala wa Israel utaendelea na vita "utaingia shimoni," na kuonya kwamba makundi ya muqawama ya kikanda yanapanga 'operesheni za kushangaza' dhidi ya Israel.

Naye kiongozi wa Hizbullah, alipongeza hatua ya mataifa matatu ya Ulaya ya Hispania, Ireland, na Norway ya kulitambua taifa la Palestina hivi karibuni.

3488475

Habari zinazohusiana
captcha