IQNA

Maombolezo ya Mashahidi

Ismail Haniyah: Raisi Raisi Aliamini Palestina ni Suala kuu la Kiislamu Ulimwenguni

12:33 - May 22, 2024
Habari ID: 3478868
IQNA - Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas , Ismail Haniyah alipongeza misimamo ya marehemu rais wa Iran Shahidi Ebrahim Raisi ya kuunga mkono Palestina.

Aliyasema hayo alipokuwa akiwahutubia mamilioni ya watu waliokusanyika mjini Tehran Jumatano asubuhi katika Swala ya Maiti ya kihistoria ya mazishi ya Rais Raisi, Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollahian, na maafisa wengine waliopoteza maisha katika ajali mbaya ya helikopta siku ya Jumapili kaskazini magharibi mwa nchi.

Haniyah amesema katika mkutano wake wa hivi punde zaidi na Raisi katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, hayati rais wa Iran alisisitiza kuwa Palestina ndio suala kuu katika ulimwengu wa Kiislamu.

Raisi aliamini kuwa muqawama ulikuwa chaguo la kimkakati la kuandaa njia ya ukombozi wa Palestina, Haniyah alisema, akimnukuu rais huyo wa zamani akisema kuwa upinzani wa Palestina ndio mstari wa mbele kwa mapambano.

Raisi alisema katika mkutano huo kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kuliunga mkono taifa la Palestina hadi wafikie lengo lao, Haniyah ameongeza.

Hayati Rais wa Iran pia ameitaja Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa kuwa ni tetemeko la ardhi ambalo liliutikisa utawala wa Kizayuni na kuanzisha mabadiliko makubwa duniani, ameongeza mkuu wa Hamas.

Rais Raisi, Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollahian, na ujumbe walioandamana nao alikufa shahidi baada ya helikopta iliyokuwa imewabeba kuanguka katika mkoa wa kaskazini-magharibi mwa Azarbaijan Mashariki Mei 19, 2024. Miili yao ilipatikana Jumatatu baada ya operesheni kubwa ya kuwasaka usiku mzima. .

Iran iko katika siku tano za maombolezo ya kitaifa huku misafara ya mazishi ya mashahidi ikiwa imepengwa katika miji mingi.

Rais Raisi anatarajiwa kuzikwa siku ya Alhamisi kwenye Haram Takatifu ya Imam Ridha (AS) huko Mashhad, kaskazini mashariki mwa Iran.

3488451

Habari zinazohusiana
captcha