IQNA

Siasa

Wagombea walioidhinishwa kugombea urais wa Iran kubainisha mipango yao kuhusu Qur'ani

10:42 - June 10, 2024
Habari ID: 3478958
IQNA-Makao Makuu ya Uchaguzi katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iran yametangaza orodha ya mwisho ya viongozi waliodhinishwa kugombea uchaguzi wa mapema wa duru ya 14 ya urais wa Jamhuri ya Kiislamu.

Six candidates were named by Iran's Interior Ministry on June 9, 2024 to run in the 14th presidential election.Mohsen Eslami, Msemaji wa Makao Makuu ya Uchaguzi ya Iran amesema shakhsia sita ndio waliodhinishwa na Baraza la Kulinda Katiba la Iran lenye wanachama 12, kuwania uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika Juni 28 hapa nchini.

Waliodhinishwa ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Sheria wa Iran, Mostafa Pourmohammadi, Waziri wa zamani wa Afya, Massoud Pezeshkian, na Amirhossein Ghazizadeh-Hashemi, Makamu wa Rais na Mkuu wa Wakfu wa Masuala ya Mashahidi na Maveterani.

Wengine waliopasishwa kugombea nafasi hiyo iliyobaki wazi baada ya kufa shahidi Rais Sayyid Ebrahim Raisi katika ajali ya helikopta Mei 19 ni Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge), Mohammad Baqer Qalibaf, Meya wa jiji la Tehran, Alireza Zakani, na Saeed Jalili, mjumbe mkuu wa zamani wa mazungumzo ya nyuklia ya Iran.

Wakati huo huo wagombea wanaowania nyadhifa katika uchaguzi wa 14 wa rais wa Iran watafafanua mipango yao katika uga wa shughuli za Qur'ani Tukufuwakati wa kampeni zao.
Haya ni kwa mujibu wa Hujjatul Seyed Mostafa Hosseini, katibu wa Baraza la Maendeleo ya Utamaduni wa Qur'ani, akizungumza na IQNA kuhusu uchaguzi ujao wa rais.
Hujjatul Islam Hosseini aliiambia IQNA kwamba wagombea hao hivi karibuni watazindua kampeni zao za uchaguzi na pia kutakuwa na midahalo kwenye televisheni ili watu wawafahamu zaidi na mipango yao.

Iran Presidential Hopefuls to Announce Their Quranic Plans
Kwa kuzingatia mapatano kati ya Sekretarieti ya Baraza la Maendeleo ya Utamaduni wa Qur'ani na Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB), ambalo litaendesha midahalo baina ya wagombea urais, imeamuliwa kuwa wagombea hao watazungumzia mipango yao ya Qur'ani, miongoni mwa mambo mengine.
Ameongeza kuwa maoni na maswali ya wanaharakati wa Qur'ani nchini yatakusanywa katika siku chache zijazo na baadhi yao yatachaguliwa kuwekwa kwa wagombea urais.

3488683

Habari zinazohusiana
captcha