IQNA

Maombolezo

Ayatullah Raisi alikuwa na shauku ya kutumikia wananchi: Mkuu wa ACECR

19:03 - May 21, 2024
Habari ID: 3478863
IQNA – Shahidi Ayatullah Ebrahim Raisi alikuwa na shauku ya kuwatumikia watu, Rais wa Akademia ya Elimu, Utamaduni na Utafiti ya Iran (ACECR) amesema.

Akizungumza na IQNA baada ya kufa shahidi rais wa Iran na wasaidizi wake katika ajali ya helikopta siku ya Jumapili, Hassan Moslemi Naeini aliangazia unyenyekevu wa Ayatullah Raisi na mapenzi yake ya kuwatumikia watu.

Alisema rais alidumisha uhusiano mzuri sana na wenzake na watu wa nchi. Ayatullah Raisi bila kuchoka aliendelea kujitahidi kwa ajili ya kuwatumikia watu wa Iran ya Kiislamu na hatimaye Mwenyezi Mungu akamjaalia baraka kubwa za kifo cha kishahidi, alisema.

Moslemi Naeini pia amezungumzia jinsi rais alivyoitazama Akademia ya Elimu, Utamaduni na Utafiti ya Iran (ACECR) akisema Ayatullah Raisi aliiona taasisi kuwa muhimu sana nchini na daima aliwakumbusha wanachama wa ACECR shughuli zao muhimu na haja ya kudumisha uhusiano na vyuo vikuu na vituo tofauti vya kitaaluma.

Rais pia aliangazia mara kwa mara shughuli za kitamaduni na sanaa za ACECR, ameainisha.

Moslemi Naeini ameendelea kusema kuwa, kama vile Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei alivyosisitiza siku ya Jumapili, njia ya utumishi ambayo Ayatullah Raisi alifuata itaendelea baada ya kufa shahidi rais na hakutakuwa na usumbufu katika masuala ya nchi.

Rais Raisi, Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollahian, Imamu wa sala ya Ijumaa wa Tabriz na gavana wa Azarbaijan Mashariki walikuwa miongoni mwa waliokufa shahidi katika tukio la kuanguka helikopta siku ya Jumapili.

Walikuwa wakirejea kutoka kwenye sherehe ya kuzindua bwawa kwenye Mto Aras na Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev wakati helikopta iliyokuwa imewabeba ilipoanguka katika msitu wa Dizmar, ulioko kati ya miji ya Varzaqan na Jolfa katika jimbo la kaskazini-magharibi mwa Iran la Azerbaijan Mashariki.

Walikufa shahidi katika ajali hiyo ya helikopta iliyotokea katika eneo la Varzghan mkoani Azerbaijan Mashariki, wakiwa katika kazi ya kuwahudumia na kuwatumikia wananchi.

 

4216967

Habari zinazohusiana
captcha