IQNA

Msiba

Mamilioni ya waombolezaji wakusanyika Tehran katika mazishi ya Shahidi Raisi na wenzake

9:15 - May 22, 2024
Habari ID: 3478866
IQNA-Mamilioni ya watu wamekusanyika katika mji mkuu wa Iran wa Tehran kushiriki katika mazishi ya Rais Ebrahim Raisi na wenzake, waliouawa shahidi katika ajali mbaya ya helikopta katika mkoa wa kaskazini-magharibi wa Azarbaijan Mashariki.

Umma umepokea majeneza ya mashahidi wanane katika Chuo Kikuu cha Tehran Jumatano asubuhi na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei ameongoza sala ya maiti na kuaga miili hiyo.

Jana waombolezaji  walihudhuria hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Imam Khomeini Mosalla wa Tehran kama sehemu ya maombolezo mwishoni mwa siku ya Jumanne kutoa heshima kwa Rais Raisi na wenzake

Mji wa kaskazini-magharibi mwa Iran wa Tabriz na mji mtakatifu wa Qom ulikuwa Jumanne asubuhi na jioni eneo la mamilioni ya watu waliokuwa walikusanyika kutoa heshima kwa mashahidi.

4217551

Habari zinazohusiana
captcha