Mamilioni ya Wairani na watu kutoka maeneo mbali mbali ya dunia wameshiriki katika Swala hiyo ambapo Kiongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, Ismail Haniya, amehutubia waombolezaji waliojawa na huzuni.
Tangu saa kumi na moja asubuhi, waombolezaji walianza kumiminika katika Chuo Kikuu cha Tehran kwa ajili ya mazishi ya marehemu Rais Raisi, Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollahian, Imamu sala ya Ijumaa wa Tabriz Ayatullah Al-e Hashem, gavana wa Azarbaijan Mashariki Malek Rahmati, Brigedia Jenerali Mousavi, walini na marobani wa helikopta..
Helikopta iliyokuwa imewabeba mashahidi hao ilianguka katika milima ya Varzaghan katika mkoa wa Azarbaijan Mashariki siku ya Jumapili. Miili ya mashahidi ilipatikana baada ya juhudi kubwa za makumi ya timu za uokoaji usiku kucha.
Shughui ya mazishi ilianza Tabriz siku ya Jumanne. Miili hiyo ilihamishiwa Qom baadaye mchana na kisha jana usiku ikawasili Tehran jana usiku.
Hapa chini ni klipu ya Ayatullah Khamenei akiongoza sala ya maiti ya mashahidi.
Shahidi Raisi anatazamiwa kuzikwa katika Haram Takatifu ya Imam Ridha (AS) huko Mashhad, kaskazini mashariki mwa Iran.