Helikopta iliyokuwa imembeba Raisi Raisi, Waziri wa Mambo ya Nje Amir-Abdollahian, kiongozi wa Swala ya Ijumaa ya Tabriz Ayatillah Mohammad Ali Al-e-Hashem, Gavana wa Azarbaijan Mashariki Malek Rahmati, kamanda wa kikosi cha usalama cha rais, marubani wawili na walinzi ilianguka mkoa wa kaskazini-magharibi wa Azarbaijan Mashariki mnamo Mei 19, 2024. Miili yao ilipatikana siku ya Jumatatu baada ya msako wa usiku mzima katika eneo lililokuwa na hali mbaya ya hewa. Waote waliokuwa katika helikopte hiyo walipoteza maisha na kupata daraja ya juu ya kufa shahidi.
Kwa mujibu wa ripoti ya pili iiliyotangazwa Jumatano na Kamati Kuu ya Kuchunguza Sababu za Ajali ya Helikopta ya Rais na ujumbe aliofuatana nao, sehemu kubwa ya nyaraka zinazohusiana na ukarabati na matengenezo ya helikopta iliyoanguka zilichunguzwa kwa makini na hakuna matatizo yoyote yaliobainika. Aidha helikopta hiyo ilikuwa imebeba abiria kwa mujibu wa uwezo wake.
Halikadhalika kulingana na mazungumzo ya mwisho yaliyorekodiwa kati ya marubani wa helikopta katika msafara na helikopta iliyoanguka hakuna tangazo la dharura lililorekodiwa.
Ripoti hiyo pia imebaini kuwa hakuna mlipuko wowote uliotokea wakati helikopta ikiwa inaruka na kabla ya kugonga mlima.
Pia imeelezwa katika ripoti kwamba kwa mujibu wa uchunguzi wa kitaalamu hakuna athari za vita vya kielektroniki kwenye helikopta iliyoanguka.
Ripoti ya awali ya Kamandi Kuu ya Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilisema uchunguzi wao wa awali umebaini kuwa, hakuna kitu chochote kisichokuwa cha kawaida kinachoweza kuhusishwa na ajali ya helikopta ya rais iliyoanguka. Ripoti hiyo ya wiki iliyopita ilibaini kuwa; "Hakuna alama zozote za kuashiria kuwa helikopta hiyo ilitunguliwa au kushambuliwa." Uchunguzi wa sababu ya kuanguka helikopta hiyo bado unaendelea.
4219140