IQNA

Mwanamuqawama

Shahidi Waziri wa Mambo ya Nje Amir-Abdollahian: Gwiji wa diplomasia ya Iran

15:36 - May 22, 2024
Habari ID: 3478870
IQNA-Katika ajali mbaya ya helikopta iliyopelekea kuuawa shahidi Rais Ebrahim Raeisi, Iran pia ilimpoteza mwanadiplomasia mwanamapinduzi na shujaa ambaye aliingiza uhai mpya katika maisha ya sera kigeni za Jamhuri ya Kiislamu katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Shahidi Waziri wa Mambo ya Nje Amir-Abdollahian: Gwiji wa diplomasia ya Iran

IQNA-Katika ajali mbaya ya helikopta iliyopelekea kuuawa shahidi Rais Ebrahim Raeisi, Iran pia ilimpoteza mwanadiplomasia mwanamapinduzi na shujaa ambaye aliingiza uhai mpya katika maisha ya sera kigeni za Jamhuri ya Kiislamu katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollahian alikuwa mtu ambaye uwezo wake wa ajabu wa kidiplomasia uliinua hadhi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika eneo na dunia.

Mwanadiplomasia huyo mkuu wa Iran aliandamana  na Rais Raisi hadi kwenye mpaka na Azerbaijan kuzindua bwawa la maji.

Wakiwa njiani kurudi, helikopta yao ililazimika kutua kwa shida kutokana na hali mbaya ya hewa. Baada ya msako wa usiku mzima, miili yao iligunduliwa alfajiri ya Jumatatu, na kulitumbukiza taifa la Iran katika majonzi.

Kazi ya diplomasia iliyozaa matunda

Shahidi Amir-Abdollahian alizaliwa mwaka wa 1964 huko Damghan, mji muhimu kihistoria katika mkoa wa kati wa Semnan. Alimpoteza baba yake alipokuwa na umri wa miaka 6 au 7, na jukumu la kusimamia familia likawa juu ya mama yake na kaka yake mkubwa.

Alianza harakati zake za masomo mnamo 1987 katika Chuo Kikuu cha Wizara ya Mambo ya Nje, na kupata digrii ya kwanza katika diplomasia.

Amir-Abdollahian alifunga ndoa mwaka wa 1994 na kuendelea na elimu yake ya juu katika Kitivo cha Sheria na Sayansi ya Siasa katika Chuo Kikuu cha Tehran, ambapo alipata shahada ya uzamili katika ‘mahusiano ya kimataifa’ mwaka wa 1996.

Katika miaka minne iliyofuata, alijishughulisha na kazi ya kidiplomasia kama Naibu Balozi wa Iran jijini Baghdad, ambako alipata ujuzi fasaha wa Kiarabu.

Aliendelea na kazi yake ya kidiplomasia akifanya kazi katika Wizara ya Mambo ya Nje, akishikilia wadhifa wa Naibu Mkuu wa Idara ya Kwanza ya Kisiasa katika Ghuba ya Uajemi kutoka 2001 hadi 2003, na kama Naibu Msaidizi Maalum wa Wizara ya Mambo ya Nje katika masuala ya Iraq miaka mitatu ijayo.

Wakati huo huo, kwa miaka miwili, alikuwa mjumbe wa Kamati ya Kisiasa-Usalama ya Timu ya Mazungumzo  ya Nyuklia baina ya Iran  nan chi za EU-3, ambazo ni Ufaransa, Ujerumani na Uingereza.

Mnamo 2006, Amir-Abdollahian alianza masomo yake ya uzamivu katika Chuo Kikuu cha Tehran, na mnamo 2010 alipata Shahada ya Uzamivu (PhD) katika 'mahusiano ya kimataifa', akionyesha kujitolea kwa ubora wa kitaaluma na uelewa wa kina wa masuala ya kimataifa.

Kando na masomo yake, alifanya kazi kwa miaka miwili kama Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Idara a Ghuba ya Uajemi, pamoja na Mkuu wa Kamati ya kuhusu Iraq katika Wizara ya Mambo ya Nje.

Mnamo 2007, alikuwa mwanachama wa timu ya mazungumzo katika mazungumzo ya pande tatu kati ya Iran, Iraq na Marekani na kutoka 2007 hadi 2010, alikuwa balozi wa Irannchini Bahrain.

Aliendelea kushika wadhifa wa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Ghuba ya Uajemi na Asia Magharibi kwa muda wa miaka miwili, na kisha kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran  wa Masuala ya Kiarabu na Afrika kwa miaka mitano.

Kabla ya kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, alifanya kazi pia kama Msaidizi Maalum wa Spika wa Bunge na Mkurugenzi Mkuu wa Masuala ya Kimataifa ya Bunge.

Amir-Abdollahian pia alihudumu kama mshauri katika Chuo Kikuu cha Tehran, Chuo Kikuu cha Allameh Tabatabai, Chuo Kikuu cha Ulinzi cha Kitaifa na Taasisi ya Uhusiano wa Kimataifa.

Pia alifanya kazi kama mhadhiri katika Kitivo cha Mafunzo ya Dunia cha Chuo Kikuu cha Tehran na Taasisi ya Uhusiano wa Kimataifa, na pia mhariri wa "Jarida la Majadiliano ya Kimkakati la Palestina" na "Utafiti Sera ya Kigeni ".

Mafanikio ya kidiplomasia ya mstari wa mbele

Wakati wa miongo mitatu ya kazi ya kidiplomasia bila kuchoka, Amir-Abdollahian alipata mafanikio mengi na popote alipojishughulisha maboresho ya mahusiano yalishuhudiwa.

Kazi yake ya kidiplomasia ilianza rasmi nchini Iraq. Utawala wa Wabaath katika nchi hiyo ya Kiarabu ulihusika na Vita vya Umwagaji damu vilivyodumu kwa miaka minane dhidi ya Iran katika muongo wa 80 lakini uhusiano huo ulipungua kwa kiasi kikubwa katika miaka ya baadaye.

Amir-Abdollahian akiwa mmoja wa wanadiplomasia wakuu wa eneo la Ghuba ya Uajemi alipewa jukumu la kufanya mazungumzo ya kubadilishana wafungwa wa mwisho wa kivita.

Mwaka 2007, kwa ombi la mamlaka mpya ya Iraq, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei alimkabidhi jukumu la mazungumzo katika mazungumzo ya pande tatu kati ya Tehran, Baghdad na Washington kuhusu suala la usalama wa Iraq.

Miaka kadhaa baadaye, Amir-Abdollahian alizungumza juu ya kutokuwa weledi wanadiplomasia wa Marekani ambao waliwasilisha madai magumu wakitarajia ridhaa kutoka upande wa pili na kuacha mazungumzo wakati hawakuwa na majibu yenye mantiki kwa hoja zenye mantiki.

Ingawa vikao vitatu vya mazungumzo havikuleta matokeo yaliyotarajiwa, viliwakilisha moja ya mazungumzo ya kwanza ya moja kwa moja kati ya wanadiplomasia wa Iran na Marekani na vilichangia kwa kiasi kikubwa uhusiano wa Iran na Iraq na kuaminiana.

Kwa usahihi zaidi, hapo awali Marekani iliona mazungumzo hayo kama ya pande mbili, lakini Iran ilisisitiza kwamba Wairaqi pia washiriki katika mazungumzo hayo kwa sababu yalikuwa juu ya usalama wa nchi yao.

Jukumu lake kama balozi nchini Bahrain lilibainishwa na kuboreka kwa kiasi kikubwa katika mahusiano baina ya nchi mbili: mikutano ya wakuu wa nchi ilifanyika Manama, makubaliano ya nishati yalijadiliwa, na pande mbili zilishiriki katika ubia mwingi wa kiuchumi.

Amir-Abdollahian alikuwa mfuasi mkubwa wa Mhimili wa Muqawama na rafiki wa karibu wa Shahidi Jenerali Qassem Soleimani, kamanda mkuu wa kupambana na ugaidi, hasa kwa vile nyanja ya kidiplomasia na kijeshi ya kiutendaji kwa nchi zote mbili zilikuwa nchi za Kiarabu.

Alichukua nafasi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran mnamo 2021 wakati Iran ikikabiliana na Marekani ambayo ilikuwa iantekeleza sera za uhasama na majaribio ya kuitenga Iran kimataifa.

Mafanikio ya kidiplomasia chini ya uongozi wake tangu wakati huo hadi leo yamekuwa makubwa, katika ngazi ya kitaifa, kieneo  na kimataifa.

Chini ya sera ya "Ujirani-Kwanza" ya Rais Raisi, alikuwa mstari wa mbele wa mikutano ya kidiplomasia na viongozi wote wa nchi jirani, kuboresha kwa kiasi kikubwa uhusiano, kuleta utulivu wa kikanda na biashara, na kusambaratisha kikamilifu vikwazo vya Marekani.

Amir-Abdollahian na mwenzake wa Saudia waliushangaza ulimwengu mwaka jana walipokubali kurejeshwa kwa uhusiano baada ya miaka mingi ya mvutano. Jitihada hizo zilifanikiwa kwa  upatanishi wa China.

Mwaka huu, kutokana na jitihada za Amir-Abdollahian Iran imefanikuwa kuwamwanachama kamili wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO), ikifuatiwa na jumuiya ya nchi zinazoibuka kiuchumi,BRICS. Hizi ni jumuiya mbili muhimu kimataifa ambazo zina nguvu na zinalenga kukuza sera ya ushirikiano wa pande kadhaa kimataifa katika kuchukua maamuzi yaani multilateralism.

Amir-Abdollahian na timu yake ya kidiplomasia pia walikuwa na nafasi muhimu katika mikutano ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC), G77 na jumuiya nyingine za kimataifa, na alifanikiwa sana kuimarisha nafasi ya Iran katika jukwaa la dunia.

Ushirikiano kuhusu suala la Palestina

Miongoni mwa masuala mbalimbali ambayo yalikuwa ajenda katika kipindi chake cha miaka mitatu ya uwaziri ni Palestina. Alijitolea muhanga katika kadhia ya Palestina na juhudi za kusimamisha na kukomesha jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina.

Katika kipindi cha miezi minane iliyopita, safari nyingi za kikanda na mashauriano za Amir-Abdollahian zilihusu suala la Palestina ambapo alitumia uwezo wake wote wa kidiplomasia kuwasaidia Wapalestina.

Mara kwa mara alisafiri hadi Iraq, Syria, Lebanon, Uturuki, Qatar na Oman, kujadili hatua za vitendo na kuratibu hatua na nchi jirani za Gaza.

Amir-Abdollahian pia alikuwa sauti ya Wapalestina katika mikutano ya mashirika mengi ya kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa, Baraza la Usalama, mikutano ya kilele ya haki za binadamu huko Geneva, pamoja na mifumo ya kimataifa kama Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa BRICS.

Mwezi Februari, alikuwa mjini Baghdad katika ziara ya kieneo wakati tu ndege za utawala wa Kizayuni zilipokuwa zikilipua eneo karibu na Damascus ili kuzuia safari zake zaidi.

Ratiba yake haikuingiliwa kwani siku hiyo hiyo ujumbe wake katika hatua ya kijasiri ulitoka Baghdad hadi Beirut, na kufanya mkutano na kiongozi wa upinzani wa Hizbullah Sayyed Hassan Nasrallah, pamoja na baadhi ya viongozi wa muqawama wa Palestina.

Amir-Abdollahian alifanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jihad Islami Ziyad al-Nakhalah, mwakilishi wa Hamas nchini Lebanon Osama Hamdan, na naibu katibu mkuu wa chama cha Harakati Kwa Ajili ya Ukombozi wa Palestina (PFLP) Jamil Mazhar.

Baada ya hapo alielekea Damascus kupitia mpaka wa nchi kavu, na kufanya mikutano na wawakilishi wa mirengo ya Wapalestina yenye makao yake mjini Damascus, wakibadilishana mawazo juu ya matukio ya hivi karibuni ya Palestina na njia za kusitisha vita vya mauaji ya halaiki dhidi ya Gaza.

Alisema utawala wa Kizayuni ulisambaratika kabisa baada ya Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa, na lau si ushiriki wa Marekani katika uwanja huo ili kuuunga mkono na kuuokoa utawala wa Kizayuni, walimwengu wangeshuhudia kikamilifu kusambaratika kwake.

Akihimiza kuwepo kwa umoja wa Wapalestina, alipongeza makundi ya muqawama nchini Lebanon, Yemen, Iraq na Syria kwa uungaji mkono wao kwa taifa la Palestina, na akapongeza uungwaji mkono mkubwa kwa Wapalestina unaofanywa na mataifa mengi duniani.

Amir-Abdollahian alionyesha tena ujasiri wake wa ajabu baada ya uvamizi wa Israel dhidi ya ofisi ya ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus, ambao ulipelekea kuuawa shahidi washauri kadhaa wa kijeshi wa Iran.

Licha ya hatari zinazoweza kutokea, alisafiri kwa ushujaa hadi Damascus na kuzuru eneo hilo, na kutuma ujumbe muhimu kwa utawala wa Kizayuni na waungaji mkono wake.

Ukosoaji wa siasa za kibeberu za Magharibi

Amir-Abdollahian pia atakumbukwa kama mpinzani mkubwa wa madola ya kibeberu ya Magharibi hasa Marekani.

Katika hafla moja, katika mkutano na wajumbe wa Ulaya, alisema wanapaswa kuishukuru Jamhuri ya Kiislamu na Shahidi Soleimani kwa kuchangia amani na usalama duniani.

"Kama kusingekuwa na Jamhuri ya Kiislamu, vituo vyako vya metro na sehemu za mikusanyiko huko Brussels, London na Paris havingekuwa salama," Amir-Abdollahian alisema wakati huo.

Kufuatia shambulio la kigaidi la Daesh la mwaka 2022 katika Haram Shah Cheragh huko Shiraz kati mwa Iranambapo raia 13 walipoteza maisha, alikosoa vikali misimamo ya baadhi ya nchi za Magharibi katika kuhimiza ugaidi na ukatili nchini Iran na kuunga mkono vita vya vyombo vya habari.

Katika kikao cha 52 cha Baraza la Haki za Binadamu kilichofanyika mjini Geneva, alieleza kuibuka ugaidi na misimamo mikali kuwa ni moja ya changamoto kuu za zama za sasa na kutoa mifano ya shambulio la kigaidi lililotajwa hapo juu huko Shiraz na kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu katika baadhi ya nchi za Magharibi.

Mwanzoni mwa mwaka huu, Amir-Abdollahian pia alilaani kimya cha baadhi ya serikali za Magharibi kuhusiana na jinai zinazofanywa na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Wapalestina wasio na hatia huko Gaza.

3488444

Habari zinazohusiana
captcha