IQNA

Maombolezo ya Mashahidi

Shughuli ya kumuaga shahidi Rais Raisi na mashahidi wenzake mjini Qum

IQNA – Shughuli ya kuaga viwiliwili vya marehemu rais shahidi wa Iran Ebrahim Raisi, wenzake waliokufa shahidi aktika ajali ya helikopta imefanyika katika mji mtakatifu wa Qum mnamo Mei 21, 2024, kwa kushirikisha mamia ya maelfu ya watu.

Rais Raisi, Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollahian, na ujumbe alioandamana nao walipoteza maisha baada ya helikopta iliyokuwa imewabeba kuanguka katika mkoa wa kaskazini-magharibi mwa Azarbaijan Mashariki kutokana na hali mbaya ya hewa Mei 19, 2024. Miili yao ilipatikana Jumatatu baada ya operesheni ya kuitafuta usiku mzima.

Iran iko katika siku tano za maombolezo ya kitaifa huku shughuli za kuwaaga mashahidi na mazishi ya mashahidi zikiwa zimepangwa katika miji kadhaa.

Leo Jumatano Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliongeza Swala ya maiti ya mashahidi katika uwanja wa Chuo Kikuu Tehran.

Habari zinazohusiana