IQNA

Usomaji wa Surah Al-Nasr kwa Sauti ya Qari kutoka Afrika ya Kati

18:57 - July 20, 2025
Habari ID: 3480972
IQNA- Ibrahim Isa Musa, qari mashuhuri kutoka Afrika ya Kati, ameshiriki katika kampeni ya Qur’ani ya “Fath” iliyoandaliwa na shirika la IQNA kwa kusoma Surah Tukufu ya Al-Nasr.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IQNA, qari huyu kijana ameshiriki kwa kutuma video ya usomaji wake wa Surah hiyo Tukufu kama sehemu ya kampeni ya Qur’ani inayolenga kueneza ujumbe wa Kiislamu na kuthamini sauti za qari kutoka maeneo mbalimbali ya ulimwengu wa Kiislamu.

Kampeni hii, iliyoanzishwa na Shirika la Kimataifa la Habari za Qurani (IQNA), inahamasisha Waislamu kushiriki kwa kusoma aya maalum za Qurani Tukufu – ikiwemo Surah Al-Fath (aya 1–4), Surah An-Nasr, na aya ya 139 ya Surah Al-Imran.

Waandalizi wanasema usomaji huu unalenga kuwa nguvu ya kiroho kwa wapiganaji walioko mstari wa mbele, na pia kukuza ujumbe wa Qurani wa subira, msaada wa Mwenyezi Mungu, na ushindi wa haki juu ya batili.

Tuma usomaji wako kwa WhatsApp kupitia nambari: +989127397608

captcha