Marzieh Afkham amesema kuwa bila shaka yoyote utawala wa Kizayuni umetenda jinai hiyo kwa kuhofia kuibuka Intifadha ya Tatu ya wananchi madhulumu wa Palestina katika ardhi zao zinazokaliwa kwa mabavu khususan muqawama wa Kiislamu katika Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan.Bi Afkham ameongeza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inatambua kuwa utawala ghasibu wa Kizayuni unahusika na kushadidisha vitendo vya ugaidi wake wa kiserikali na hivyo kuzitaka taasisi za kimataifa khususan Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kulaani jinai hiyo na kuwajibika ili kuzuia kuendelezwa jinai za Wazayuni dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina walio chini ya mzingiro huko Ghaza.
Ndege za kivita za utawala wa Kizayuni jana zilifanya mashambulizi katika maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Ghaza na kuwaua shahidi na kuwajeruhi raia kadhaa wa Palestina wa eneo hilo. Duru za Palestina pia zimeripoti kujiri mashambulizi ya ndege za Israel aina ya F-16 huko magharibi mwa Khan Yunis kusini mwa Ukanda wa Ghaza na katika eneo la al Barij huko huko Ghaza pia.
1346565