IQNA

Khatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran

Utawala ghasibu wa Israel umeshindwa vibaya Gaza na uhalali wake umetiwa doa katika uga wa kimataifa

23:38 - October 10, 2025
Habari ID: 3481350
IQNA-Khatibu wa Swala ya Ijumaaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, miaka miwili baada ya Operesheni kubwa ya Kimbunga cha Al-Aqswa haiba ya utawala wa Kizayuni imejaa msukosuko na mparaganyiko.

Hujjatul-Islam wal-Muslimin Mohammad Javad Haj Ali Akbari amesema hayo leo mbele ya hadhara ya waumini waliohudhuria ibada ya Swala ya Ijumaa mjini Tehran na kubainisha kwamba, katika miaka hii miwili, utawala ghasibu wa Israel umeshindwa vibaya sana, uhalali wake umetiwa doa katika uga wa kimataifa, na genge linalochukiwa zaidi duniani ni utawala wa Kizayuni.

Walitaka kutekeleza Mpango wa Abraham ambao ulishindikana, na kushindwa kwao pakubwa ni makubaliano ya kusitisha vita ambayo wamelazimika kuyakubali huku wakiwa hawajatimiza matakwa yao yoyote.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema, awali utawala wa kizayuni wa Israel ulikuwa ukizungumzia kuiangamiza Hamas, lakini umelazimika kujadiliana na na harakati hiyo ya muqawama.

Sheikh Haj Ali Akbar ametahadharisha kwamba, adui Mzayuni hawezi kuaminiwa kwa hali yoyote ile, na kila mtu aliye katika upande wa kambi ya muqawama lazima awe mwangalifu, na Hamas na Jihad lazima zijiweke tayari. Lakini inachekesha kuona kwamba Trump anajiona kama mjumbe wa amani, ilihali ukweli wa mambo yeye ni mtuhumiwa  nambari moja katika mauaji ya kimbari huko Gaza.

Ama kuhusiana na madai ya Ulaya kuhusu visiwa vitatu vya Iran, Khatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran amesema: Tunayaambia madola ya Ulaya kwamba, visiwa hivyo vitatu vya Tomb Kubwa, Tomb Ndogo, na Buu Musa vilikuwa mali ya Iran, ni vya Iran na vitaendelea kuwa mali ya taifa hili.

4309850

captcha