Kwa mujibu wa Ahmad Ibsais, Mmarekani wa kizazi cha kwanza mwenye asili ya Kipalestina na mwanafunzi wa sheria, katika makala yake kwa Al Jazeera:.“...utukufu kwa watu wa Palestina, kwa ustahimilivu wao na nguvu yao ya pamoja. Wapalestina walikataa kunyenyekea kwa simulizi iliyowekwa juu yao — kwamba wao ni ombaomba wanaotafuta msaada, ‘magaidi’ wanaopaswa kulipa, au chochote kilicho chini ya hadhi ya watu wanaostahili kuheshimiwa bila masharti wala dharau.”
“Mpango wa ‘amani’ wa Trump ulizikwa pamoja na kila mtoto wa Gaza, kila familia iliyofurushwa, na kila siku dunia ilipoita mauaji ya halaiki ‘kujilinda’ — ikipuuzia uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki wa mwaka 2004 kwamba mkoloni hawezi kudai kujilinda dhidi ya waliokaliwa.”
Mustakabali wa haki ni uhuru kamili — taifa moja la kidemokrasia lenye haki sawa kwa wote, likianzia na haki ya Gaza kuamua hatima yake bila mzingiro, bila ukaliaji na bila udhibiti wa kigeni unaojificha kama walinda amani.
Lakini kwanza, watu wa Gaza wamepata haki ya kuomboleza, kuhesabu waliokufa na kuwazika kwa heshima. Zaidi ya yote, wamepata haki ya kufurahia furaha hii ndogo. Kupitia mateso yasiyoelezeka, Wapalestina wamepata haki ya kufasiri uhuru kwa mtazamo wao. Dunia haina mamlaka ya kuwaambia vinginevyo.
Muqawama ni Imara
Baada ya kutangazwa makubaliano ya usitishaji vita katika Ukanda wa Ghaza na ya kubadilishana mateka kati ya utawala wa Kizayuni wa Israel na Harakati ya Muqawama (mapambano) wa Kiislamu ya Palestina HAMAS, vyombo vya habari na duru za kisiasa za ndani ya utawala wa kizayuni zimetoa lawama kwa kuashiria matokeo ya vita na kuendelea kubaki thabiti miundo na mihimili ya Muqawama ndani ya Ghaza.
Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vimetoa makala na maandiko kadha wa kadha vikionyesha kutoridhishwa na matokeo ya vita dhidi ya Ukanda wa Ghaza baada ya kufikiwa makubaliano ya usitishaji mapigano na vimepinga kuendelea kuwepo Muqawama wenye uwezo katika eneo hilo.Yariv Levin, naibu waziri mkuu na waziri wa sheria wa utawala wa Kizayuni, ndiye aliyeko katika mstari wa mbele kwa wakosoaji na ameyaelezea makubaliano hayo kuwa ni kitu chenye "gharama kubwa mno" na akasema: "kuwaachilia huru Wapalestina kuna gharama kubwa mno.
Sisi tutaendelea kufanya juhudi ili kuhakikisha Hamas haiwi tena na silaha wala udhibiti wa Ghaza".Katika mjibizo liliotoa kwa matamshi ya Levin, jukwaa moja la habari la utawala wa kizayuni limeandika: "hadithi ilianzia kwenye kuangamizwa Hamas hadi kupokonywa silaha... lakini kwa maneno mengine ni kwamba, Hamas inasalia Ghaza."
Jukwaa hilo limetumia lugha hiyo ya mafumbo na kejeli kutoa mjibizo kwa kauli ya naibu waziri mkuu huyo na waziri wa sheria wa utawala wa kizayuni.
3494945/