IQNA

Mradi wa Kitaifa wa Kusahihisha Usomaji wa Qur'an Wazinduliwa Misri

18:19 - October 11, 2025
Habari ID: 3481351
IQNA – Mradi wa kitaifa uitwao Miqraat al-Majlis (Usomaji wa Kikao) umezinduliwa nchini Misri kwa lengo la kusahihisha usomaji wa Qur'an Tukufu.

Mpango huu unalenga kuwafundisha washiriki usomaji sahihi wa aya za Qur'an Tukufu, kusahihisha matamshi, na kuwasaidia kuimudu kanuni za Tajwidi.

Baraza Kuu la Mambo ya Kiislamu nchini Misri ndilo lililoanzisha mradi huu, kwa nia ya kuhudumia Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kueneza elimu yake miongoni mwa watu.

Mradi huu unatekelezwa ndani ya mkakati wa Baraza wa kupanua utamaduni wa Qur'ani na kurahisisha njia za kujifunza usomaji sahihi kupitia mikutano ya kielimu ya kuingiliana moja kwa moja.

Katika mikusanyiko hii, washiriki hufundishwa kusahihisha matamshi yao na kusoma kwa njia sahihi, huku wakifahamishwa misingi ya elimu ya Tajwidi ili kuufanya usomaji wao kuwa wa ukamilifu na uadilifu.

/3494950/

Mikusanyiko hiyo hufanyika chini ya kauli mbiu: "Sahihisha matamshi yako na upambe usomaji wako kwa Miqraat al-Majlis."

Sheikh Marwan Yahya, ambaye ni mjumbe wa Kitengo cha Mawasiliano ya Baraza hilo, hutoa mafunzo ya usomaji sahihi wa Qur'ani katika vipindi hivyo.

Aidha, Baraza hilo linajitahidi kutumia vyombo vya habari vya Kiislamu kuhudumia Qur'ani, kurahisisha njia za kuifundisha, na kuunganisha vizazi na Kitabu cha Mwenyezi Mungu kupitia usomaji, tafakuri, na kutekeleza mafundisho ya Qur'ani.

 

Kishikizo: misri qurani tukufu
captcha