IQNA

Anti Babaka watumia sumu kuwaua Waislamu CAR

17:28 - April 09, 2014
Habari ID: 1392667
Kundi lenye misimamo mikali ya Kikristo la Anti Balaka sasa limeanza kutumia mbinu mpya kwa ajili ya kuua Waislamu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa kuwauzia vyakula vyenye sumu. Hadi sasa makumi ya watoto wadogo wameripotiwa kufariki dunia katika mji wa Buda kutokana na mbinu hiyo ya mauaji.

IQNA imenukuu mtandao wa rfi.fr kutoka katika mji wa Buda ulioko umbali wa kilimita 180 kutoka Bangui kwamba makumi ya Waislamu wameuawa kwa umati kutokana na kula chakula kilichotiwa sumu na wafuasi wa kundi la Kikristo la Anti Balaka.
Wakazi wa mji huo wamesema kwamba baada ya kuona watoto wao wakifariki dunia kutokana na kutumia baadhi ya vyakula, walifanya uchunguzi na kubaini kuwa kundi la Anti Balaka linawalazimisha wamiliki wa maduka ya mji wa Buda kuwauzia Waislamu vyakula vyenye sumu kwa lengo la kuwamaliza kabisa wafuasi wa dini.
Wakati huo huo Shirika la Habari la Ufaransa limemnukuu ripota wake katika Jamhuri ya Afrika ya Kati akisema kwamba wanachama wa kundi la Kikristo la Anti Balaka wamepiga marufuku kuuziwa Waislamu matunda na vyakula na kwamba mfanya biashara yeyote anayekiuka amri hiyo anauawa.
Wafuasi wa kundi hilo wanasema Waislamu wanapaswa kuondoka katika Jamhuri ya Afrika ya kati la sivyo watakufa kwa njaa.
Baadhi ya Waislamu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wameliambia Shirika la Hahari la Ufaransa kwamba awali wanachama wa kundi la Anti Balaka walikuwa wakiwaua kwa umati Waislamu kwa kutumia silaha moto lakini sasa wamebadili mbinu zao na wanawaua wafuasi wa dini hiyo kwa kutumia sumu. Wanasema kuwa hadi sasa makumi ya Waislamu hususan watoto wadogo wameuawa kwa mbinu hiyo ya kupewa chakula chenye sumu.

1391805

Kishikizo: balaka bangui waislamu sumu
captcha