IQNA

Gazeti la Kifaransa lililomdhalilisha Mtume lapigwa marufuku Tunisia

11:48 - November 05, 2008
Habari ID: 1704814
Wizara ya Mambo ya Nje ya Tunisia imepiga marufuku gazeti la "Le'Express International" kwa sababu ya kumvunjia heshima Mtume wa Uislamu, Muhammad SAW na matukufu ya Kiislamu.
Kituo cha habari cha Zawya kimemnukuu afisa mmoja wa ngazi za juu wa serikali ya Tunisia akisema kuwa, Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo ina haki ya kupiga marufuku uuzaji wa jarida lolote la kigeni linalovunjia heshima Uislamu kwa mujibu wa mada ya 25 ya hati ya sheria za vyombo vya habari.
Ijumaa iliyopita Wizara ya Habari ya Morocco pia ililipiga marufuku jarida hilo kwa sababu ya kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu.
Hata hivyo Mhariri wa Le' Express International Christian Macrin amesema kuwa hatambui maana ya uamuzi huo wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Morocco akidai kwamba, picha iliyodaiwa ni ya Mtume Muhammad iliyochapishwa juu ya jarida hilo imeonyeshwa nusu kama ishara ya kuheshimu itikadi za Waislamu wa Morocco.
Chini ya picha hiyo kuna maandishi yanayosomeka: "Mgongano, ujumbe, mwenendo na mtazamo wa Muhammad na Masihi" 315612
captcha