Huku akitangaza habari hizo kupitia njia ya simu na Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa IQNA, Hujjatul Islam wal Muslimeen Muhammad Asadi Muwahhid, mkuu wa kitengo hicho amesema kuwa hutoba na uwasilishaji makala ni sehemu muhimu ya ajenda ya warsha hiyo ya siku moja. Amesema kuwa makala na hotuba zitakazotolewa katika warsha hiyo zitalenga kutoa mtazamo na mafundisho halisi ya Uislamu na sio mitazamo potofu inayowasilishwa na makanisa kwa ajili ya kuuharibia jina Uislamu. Amesema, warsha hiyo ambayo itahudhuriwa na wanachuo wanaosomea masuala ya kidini na ambao baadaye watakuwa walimu katika uwanja huo, itajadili masuala mbalimbali yakiwemo ya haki za binadamu, nafasi ya mwanamke katika Uislamu na uhuru katika Uislamu. Amesema maonyesho maalumu ya kanda, cd na vitabu vya Kiislamu vilivyoandikwa na kutarjumiwa katika lugha za Kiingereza, Kifaransa, Kiswahili na lugha nyingine yataandaliwa pambizoni mwa warsha hiyo ili kuwafahamisha wasomaji, wasikilizaji na watazamaji mafundisho ya Kiislamu. Hujjatul Islam Wal Muslimeen Muhammad Asadi Muwahhid ni miongoni mwa shakhsia watakaotoa hotuba katika warsha hiyo. Hotuba yake itahusu masuala na mafundisho mbalimbali tunayopata kutokana na Qurani na vilevile athari zake katika maisha ya mtu binafsi na ya kijamii ya wanadamu. 317130