IQNA

Israel yatumia maafisa wenye misimamo mikali ya Kiyahudi kwa doria katika Msikiti wa Al‑Aqsa

22:45 - June 05, 2026
Habari ID: 3482325
IQNA – Eneo takatifu na muhimu kwa Waislamu katika mji mtukufu wa al‑Quds (Jerusalem) litaanza kusimamiwa na maafisa wa polisi wenye misimamo mikali wa Kiyahudi wa mrengo wa kulia.

Polisi wa Israel wameanzisha kampeni ya uajiri inayolenga Wayahudi wenye misimamo mikali ya kidini, wakiwemo watu wanaoshiriki katika kuvamia eneo la Msikiti wa Al‑Aqsa, kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa na gazeti la Israel Haaretz.

Ripoti hiyo ilisema kuwa Daniel Lerch, naibu kamanda wa kikosi cha polisi kinachosimamia eneo la Msikiti wa Al‑Aqsa, alisambaza wito wa uajiri kupitia mitandao ya kijamii na makundi ya WhatsApp, yakiwemo makundi yanayodaiwa kujumuisha wanaharakati wa walowezi na watu wa mrengo mkali wa kulia.

Katika ujumbe wa uajiri uliotajwa na Haaretz, Lerch aliandika:

“Tumeanzisha mradi wa kuajiri maafisa wa polisi wa kidini kwa ajili ya Mlima wa Hekalu (Temple Mount). Yeyote anayetaka kushiriki katika kutekeleza mamlaka ya utawala anakaribishwa kuwasiliana nami.”

Kwa mujibu wa gazeti hilo, baadhi ya wanaharakati wanaounga mkono hujuma  za walowezi katika eneo la Msikiti wa Al‑Aqsa wamesema kuwa marabi wamewahimiza wanafunzi wao kujiunga na kikosi cha polisi kilichopewa jukumu la kusimamia eneo hilo, ili kuongeza kile walichokiita uwepo wa Kiyahudi miongoni mwa maafisa wanaolinda eneo hilo.

Ripoti hiyo iliongeza kuwa wanaharakati kadhaa wa kidini wanaoshiriki mara kwa mara katika kuvamia eneo la msikiti huo wamejiunga na jeshi la polisi katika kipindi cha mwaka uliopita.

Haaretz pia ilinukuu vyanzo vya polisi vikisema kuwa maafisa wanaofanya kazi katika maeneo ya kidini ndani ya Mji wa Kale wa al‑Quds hudumisha mawasiliano ya mara kwa mara na waziri wa usalama wa taifa wa utawala wa Israel, Itamar Ben‑Gvir, pamoja na mke wake.

3497720

Habari zinazohusiana
captcha