IQNA

Misafara ya mazishi ya Shahidi Imam Khamenei kufanyika Tehran, Qom na Mashhad

17:58 - June 03, 2026
Habari ID: 3482320
IQNA – Misafara ya mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, inatarajiwa kufanyika katika miji mitatu ya Iran, kwa mujibu wa taarifa ya afisa mmoja.

Naibu meya wa Tehran alisema katika kikao cha Tume ya Utamaduni na Masuala ya Kijamii ya Miji Mikuu ya Iran kwamba siku tatu zimetengwa kwa ajili ya shughuli za mazishi ya kiongozi huyo shahidi.

Mohammad Amin Tavakkolizadeh aliongeza kuwa misafara ya mazishi itafanyika katika miji ya Tehran, Qom na Mashhad.

“Tunajiandaa kupokea idadi ya watu kati ya milioni 15 hadi 20 katika msafara utakaofanyika katika mji mkuu.”

Tavakkolizadeh alieleza kuwa hafla ya mazishi itadumu angalau saa 24, na mahali panapotarajiwa kufanyika ni Msalla wa Imam Khomeini (RA) au Haram ya Imam Khomeini kusini mwa Tehran.

Alisema kuwa kwa mujibu wa wasia wake, mwili wa kiongozi huyo shahidi utazikwa katika Haram Tukufu ya Imam Ridha (AS) mjini Mashhad.

Aliendelea kusema kwamba kuna uwezekano wa waombolezaji kutoka Pakistan, Afghanistan, India na Bangladesh kuhudhuria msafara wa maombolezo mjini Mashhad, na kuongeza kuwa pia inatafakariwa uwezekano wa kufanya shughuli za maombolezo ya kiongozi huyo shahidi nchini Iraq.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei aliuawa shahidi katika siku ya kwanza ya vita vya kigaidi vya Marekani na utawala haramu wa Israel dhidi akiwa katika ofisi yake mjini Tehran tarehe  10 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani sawa na 28 Februari mwaka huu.

3497698

Kishikizo: imam khamenei shahidi
captcha