
Katika taarifa iliyotolewa mapema leo Jumamosi, IRGC imesema kwamba saa saba na nusu usiku wa kuamkia leo, meli nne za mafuta zilizokiuka sheria, zilizochochewa na kuongozwa na jeshi la Marekani na bila kufanya uratibu au kuzingatia maonyo ya mara kwa mara ya Jeshi la Wanamaji la IRGC, zilijaribu kuondoka kinyume cha sheria kwenye Mlango-Bahari wa Hormuz.
Taarifa hiyo imesema kufuatia maonyo ya IRRG, moja ya meli za mafuta ililengwa na kusimamishwa, na meli nyingine zilizokiuka sheria zimelazimika karudi nyuma, imesema.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kufuatia tukio hili, saa nane na nusu usiku, ndege zisizo na rubani za Marekani zimeshambulia mnara wa mawasiliano kwenye Kisiwa cha Qeshm na mnara mwingine huko Sirik kwa makombora mawili.
Imeongeza kuwa katika kukabiliana na uchokozi huo wa jeshi la Marekani, Kikosi cha Anga cha IRGC kimeshambulia kwa makombora ya balestiki kambi mbili za anga za Marekani huko Kuwait, mojawapo ikiwa ni ile ya Ali Al Salem, pamoja na vituo muhimu vilivyobaki vya Kikosi cha Tano cha Marekani huko Bahrain.
IRGC pia imemuonya "adui muovu anayeua watoto kwamba ikiwa vitendo hivyo viovu vitarudiwa, majibu yatakuwa makubwa zaidi."
"Utawajibika kwa matokeo ya kufungwa kabisa kwa Mlango-Bahari wa Hormuz kwa usafirishaji wa mafuta na gesi yako," taarifa hiyo iliongeza.
/3497730