IQNA

Chuo Kikuu cha Punjab chapinga hatua ya Wazayuni ya kuivunjia heshima Qur’ani

12:57 - November 09, 2008
Habari ID: 1706170
Wanafunzi wa Kiislamu wa Chuo Kikuu cha Punjab nchini Pakistan wamefanya mgomo wa kuketi chini mbele ya msikiti wa chuo hicho wakilaani kitendo cha askari wa utawala ghasibu wa Israel cha kuivunjia heshima Qur’ani Tukufu katika mji wa al al Khalil huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
Baada ya kutekeleza ibada ya swala ya Ijumaa, wanafunzi hao waliokuwa na mabango yenye maandishi dhidi ya Israel walichoma moto bendera ya utawala huo ikiwa ni ishara ya kuonyesha malalamiko yao dhidi ya kitendo hicho.
Wanafunzi hao wameitaka serikali ya Pakistan kuakisi malalamiko yao dhidi ya kuvunjiwa heshima Qur’ani katika nyanja za kimataifa.
Ijumaa iliyopita askari wa utawala ghasibu wa Israel walishambulia kambi ya wakimbizi wa Kipalestina ya al Arub katika mji wa al Khalil na kurarua kitabu kitukufu cha Qur’ani. Askari hao wa Kizayuni pia waliwatia nguvuni raia kadhaa wa Palestina.
Katika shambulizi lao la mwezi uliopita huko kaskazini mwa mji wa al Khalil, askari wa utawala ghasibu wa Israel vilevile walikivunjia heshima kitabu kitukufu cha Qurr’ani. 317112
captcha