IQNA

Ombi la kuasisiwa kituo cha Kiislamu Ubelgiji kuchunguzwa

12:45 - November 16, 2008
Habari ID: 1708746
Jumuiya ya Kiislamu ya Uturuki imeamua kuchunguza ombi la kuasisisi kituo cha Kiislamu nchini Ubelgiji katika eneo la Saint Vicente katika mji wa Evere.
Mpango huo mkubwa ambao lengo lake kuu ni kutoa mafunzo ya teolojia ya Kiislamu, ni sehemu ya mipango mingine kadhaa inayochunguzwa na Jumuiya ya Kiislamu ya Uturuki ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule, ukumbi wa mikutano, klabu ya michezo na shule ya chekechea.
Uchunguzi wa maombi hayo ya kuasisi kituo cha Kiislamu nchini Ubelgiji utaanza tarehe 20 mwezi huu wa Novemba. 320557
captcha