Gazeti la Arab News limeandika kuwa, Ewa Björling, Waziri wa Biashara wa Sweden ametoa pendekezo hilo katika mazungumzo yake na Zedhal Aliridha, waziri mwenzake wa Saudi Arabia na kuongeza kuwa kuimarishwa kwa uhusiano wa nchi za Kiislamu na Umoja wa Ulaya kutasaidia kurekebisha sura mbaya na potofu ya wazungu kuhusiana na Uislamu na Waislamu. Katika kuendelea na mazungumzo hayo, waziri huyo amesema kuwa picha waliyonayo watu wa Ulaya kuhusiana na ulimwengu wa Kiislamu si sahihi hata kidogo na kwamba, kuongezeka kwa mazungumzo kati ya pande mbili hizi yanaweza kusaidia sana kurekebisha jambo hilo, Mazungumzo hayo yalifanyika Jumamosi kati ya nchi hizo katika Ofisi ya Kibiashara ya Saudi Arabia huko mjini Jeddah kwa ajili ya kuongeza kiwango cha miamala ya nchi hizo katika nyanja za kibiashara. 327826