IQNA

Kongamano la kimataifa la Kutambulisha Uislamu laanza Makka

15:03 - December 01, 2008
Habari ID: 1714698
Kongamano la tisa la kimataifa la "Kutambulisha Uislamu Katika Nchi Zisizokuwa za Kiislamu; Ukweli wa Mambo na Mustakbali" limeanza kazi zake mjini Makka, Saudi Arabia.
Kongamano hilo linasimamiwa na Mfalme wa Saudia Abdullah bin Abdulaziz na linahudhuriwa na maulama, wanafikra na wahadhiri wa vyuo vikuu kutoka nchi za Kiislamu.
Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Uislamu Abdullah al Turki amesema kuwa miongoni mwa ajenda za kongamano hilo ni kuchunguza juhudi zilizofanyika katika kuarifisha misingi ya Uislamu kwa wasiokuwa Waislamu, changamoto na vizuizi vya maendeleo ya kulingalia Uislamu katika nchi zisizokuwa za Waislamu na mustakbali wa ulinganiaji Uislamu.
Al Turki amewataka wanafikra na wanazuoni wanaoshiriki katika kongamano hilo kuchunguza njia za kuimarisha mazungumzo na jinsi ya kuamiliana na wasiokuwa Waislamu na kuwapa maarifa juu ya misingi sahihi ya Uislamu.
Kongamano la kimataifa la Kuarifisha Uislamu Katika Nchi Zisizokuwa za Kiislamu hufanyika kila mwaka wakati wa msimu wa Hija huko Makka na kuhudhuriwa na mahujaji wengi wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu. 327866

captcha