
Kwa mujibu wa RT Arabic, sherehe ya ufunguzi huo ilihudhuriwa na maelfu ya Waislamu kutoka maeneo mbalimbali ya Russia.
Hili lilikuwa tukio muhimu lililoimarisha hadhi ya kidini na kitamaduni ya Waislamu wa eneo hilo.
Mashindano ya Qur’ani yaliandaliwa katika mfumo wa mashindano ya kitaifa ya kuhifadhi Qur’ani nchini Russia, na katika hafla hiyo pia iliswaliwa Swala ya kwanza ya jamaa ndani ya msikiti huo.
Wakati huohuo, Mufti wa Jamhuri ya Karachay-Cherkessia alikitunuku rasmi kituo hicho cha kidini hadhi ya “Msikiti Mkuu" au "Msikiti wa Jamia.”
Sherehe hiyo ilihudhuriwa na maelfu ya wageni kutoka sehemu mbalimbali za Russia pamoja na wawakilishi wa taasisi mbalimbali za Kiislamu na kijamii. Miongoni mwa waliohudhuria alikuwa Sheikh Suleiman Samidinov, mwakilishi wa Mamlaka ya Kidini ya Waislamu wa Jamhuri ya Crimea na mji wa Sevastopol, ambaye pia ni Imamu wa Wilaya ya Krasnogvardeysky na Mkuu wa Shule ya Kuhifadhi Qur’ani iliyo chini ya Mamlaka ya Kidini ya Waislamu wa Crimea na Sevastopol.
Katika hotuba yake, Sheikh Suleiman Samidinov alisisitiza umuhimu wa umoja wa jamii ya Kiislamu na kuhifadhi maadili ya dini yaliyo sahihi, akisema kuwa msikiti huo hautakuwa tu mahali pa kuswali, bali pia utageuka kuwa kituo cha elimu ya dini, shughuli za kheri na huduma za kijamii.
3497632