IQNA

Mstahiki Meya wa New York Mamdani alaani vita vya Marekani dhidi ya Iran, asema lazima viishe

18:04 - May 29, 2026
Habari ID: 3482297
IQNA – Mstahiki Meya wa Jiji la New York, Zohran Mamdani, amelaani vikali vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran akivitaja kuwa ni mgogoro usio na msingi, na kusisitiza kuwa vita hivyo ni lazima viishe mara moja kwa ajili ya usalama wa raia wa mataifa mengine, na pia kwa manufaa ya Wamarekani wanaopambana na hali ngumu ya maisha nyumbani kwao.

Katika ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wa X, Mamdani amesema vita hivyo vilianza miezi mitatu iliyopita na tayari vimesababisha hasara kubwa ya maisha ya watu na athari mbaya za kiuchumi.

“Maelfu ya raia wamepoteza maisha yao,” aliandika Mamdani, na kuongeza kuwa “wanajeshi kumi na watatu wa Marekani hawatarudi tena nyumbani kwa familia zao.”

Aidha, alihusisha mzozo huo na shinikizo linalozidi kuongezeka la kiuchumi ndani ya Marekani, akitolea mfano kupanda kwa bei za mafuta na bidhaa za vyakula.

Mamdani amewatuhumu viongozi wa Marekani kwa kuanzisha vita hivyo bila idhini ya Bunge (Congress), akisema kuwa Wamarekani sasa wanabeba mzigo wa matokeo ya maamuzi ambayo hawakushirikishwa kuyaafiki.

“Kila maisha yanayopotea nje ya nchi na kila dola inayokamuliwa kutoka kwa familia za wafanyakazi hapa nchini, ni sehemu ya gharama ya maamuzi haya ya hovyo,” alihitimisha.

3497636

Habari zinazohusiana
captcha