IQNA

Mashindano ya Qur’ani ya Afrika Kusini kufanyika mwezi huu

12:44 - December 04, 2008
Habari ID: 1715787
Mashindano ya Qur’ani ya Afrika Kusini yanatarajiwa kuanza tarehe 15 hadi 21 za mwezi huu wa Disemba katika mji wa Cap Town. Mashindano hayo yatasimamiwa na Jumuiya ya Qur’ani ya Afrika Kusini.
Jumuiya hiyo imetangaza kwamba mashindano hayo yatafanyika katika sekta tatu za kusoma Qur’ani, utafiti wa masuala ya Qur’ani na wahudumu bora zaidi wa kitabu hicho kitukufu.
Jumuiya ya Qur’ani ya Afrika Kusini imetoa fomu kwa watu wanaotaka kushiriki kwenye mashindano hayo kupitia mtandao wake wa intaneti wenye anwani ifuatayo: quranunion.co.za 329650
captcha