Jamal al Khidhari amesema: Kupeleka misaada ya kibinadamu kwa raia wa Palestina wanaozingira katika Ukanda wa Gaza ni katika haki zao za kimsingi na kwamba upinzani wa utawala ghasibu wa Israel dhidi ya hatua hiyo unakiuka sheria za kimataifa.
Al Khidhari amesisitiza kwamba iwapo nchi za Kiislamu zitakuwa na azma ya kweli zinaweza kuvunja mzingiro wa Gaza na kuutokomeza utawala haramu wa Israel. Mwenyekiti wa Kamati ya Wananchi ya Kukabiliana na Mzingiro wa Gaza amesema: Utawala wa Kizayuni wa Israel unajua vyema kwamba nchi za Kiarabu na Kiislamu zina uwezo mkubwa ambao iwapo utatumiwa vizuri unaweza kuuangamiza utawala huo. 332672