Mufti huyo ameyasema hayo baada ya kuwatembelea majeruhi wa Kipalestina ambao wamefikishwa nchini Misri kwa ajili ya kupata matibabu. Amesema, mauji hayo ni mabaya zaidi dhidi ya jamii ya mwanadamu kwa sababu yanawaadhibu kinyama na kwa umati watu wasio na hatia.
Wakati huohuo, Baraza la Chuo Kikuu cha al-Azhar lemeafiki pendekezo la wanachama elfu 12 wa Bodi ya Elimu ya chuo hicho kwa ajili ya kukatwa mishahara yao ya siku moja ili kuwasaidia wananchi madhlumu wa Palestina.
Katika upande wa pili, washiriki wa kikao cha kimataifa cha Jumuiya ya Kimataifa ya Wanachuo Waliohitimu Masomo yao katika Chuo cha al-Azhar, ambacho kilimalizika hivi karibuni, wamelaani mauaji na jinai za kibaguzi za Wazayuni dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza na kuzitaka jumuiya za Kiarabu na kimataifa kufanya juhudi za kusimamishwa mara moja jinai hizo. 346319