IQNA

Ban Kii Moon ataka kusimamishwa haraka mauaji ya kizazi huko Gaza

11:27 - January 14, 2009
Habari ID: 1730802
Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameutaka utawala haramu wa Israel kusimamisha mara moja mauaji yake ya umati dhidi ya wananchi wa Palestina wakazi wa Ukanda wa Gaza kwa kuheshimu na kutekeleza azimio nambari 1860 la Baraza la Usalama.
Kwa bahati mbaya, katibu mkuu huyo, hata baada ya kuendelea mauaji hayo ya kizazi dhidi ya watu wasio na hatia kwa kipindi cha wiki tatu sasa, lakini ametosheka tu kwa kuutaka utawala wa Israel usimamishe mauaji hayo ya umati bila ya kuchukua hatua zozote za maana za kuulazimisha utawala huo ufanye hivyo.
Akizungumza jana mbele ya waandishi habari huko New York, makao makuu ya Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon ameutaka utawala haramu wa Israel usimamishe mara moja mashambulio hayo katika Ukanda wa Gaza na kuruhusu kuingizwa katika ukanda huo misaada ya kibinadamu zikiwemo suhula za kitiba. Amesema kuwa, raia wengi, na hasa watoto na wanawake, wamepoteza maisha yao katika mashambulio hayo ya Israel na kwamba hivi sasa wakazi wa ukanda huo wanakabiliwa na matatizo makubwa.
Ban Ki-moon amesema kuwa utawala wa Israel hauheshimu Azimio la Geneva kuhusiana na haki za binadamu wala kulinda maisha ya raia katika maeneo ya vita. Ameendelea kusema kuwa hadi sasa utawala huo unalipua na kubomoa ovyo misikiti, shule, nyumba za makazi, majengo muhimu na miundombinu ya Ukanda wa Gaza.
Ban Ki-moon hivi sasa anazitembelea nchi saba za Mashariki ya Kati kwa ajili ya kutafuta njia za kutatua mgogoro huo. 347481
captcha