IQNA

Wanawake walioshinda katika mashindano ya Quran Kuwait wazawadiwa

10:12 - January 15, 2009
Habari ID: 1731194
Sherehe za kuwazawadia wanawake waliofuzu katika mashindano ya kwanza ya kitaifa ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu maaulumu kwa wanawake nchini Kuwait zilifanyika jana katika mji wa Qadisiya nchini humo.
Kwa mujibu wa Shirika Rasmi la Habari la Kuwait KUNA, katika sherehe hizo wanawake 13 wamekabidhiwa zawadi nono kwa kutokana na juhudi zao za kuhifadhi Qur'ani Tukufu. Mashindano ya kwanza ya kuhifadhi Quran tukufu kwa ajili ya wanawake ya "Sabihat Hussein" yalifanyika Kuwati kuanzia tarehe 2-5 Januari kwa hisani ya Kamati ya Qur'ani Tukufu inayofungamana na Jumuiya ya Mwamko wa Kiislamu ya Mji wa Qadisiya.
Wanawake 117 walishiriki katika kuhifadhi na kusoma Qur'ani katika mashindano hayo yaliyofanyika kwa ajili ya watu walio na umri wa miaka 22 kwenda juu.
Mashindano hayo yalishirikisha sekta tano za kuhifadhi juzuu tano, kuhifadhi juzuu nne kuhifadhi juzuu tatu, kuhifadhi juzuu mbili na kuhifadhi juzuu moja na tajwidi ya mojawapo ya sura za Qur'ani.
Bi Fatima Hussein Mwenyekiti wa Kamati ya Qur'ani ya Jumuiya ya Mwamko wa Kiislamu ya Qadisiya amezungumza katika hafla ya kuwazawadi washindi na kutoa wito kwa wanawake washiriki kujitahidi kuifahamu Qur'ani ipasavyo. 348329
captcha