IQNA

Papa awasamehe maaskofu wa Kikatoliki waliokana holocaust

11:52 - January 29, 2009
Habari ID: 1737417
Kiongozi wa Wakatoliki Duniani Papa Benedict wa XVI amewasamehe maaskofu kadhaa wa Kanisa Katoliki waliokana ngano ya kubuni ya Holocaust.
Papa Benedict ametoa ujumbe akitangaza msamaha kwa askofu Richard Williamson na wenzake watatu ambao wanafuatiliwa na vyombo vya sheria kwa sababu ya kukana madai ya holocaust au mauaji ya mamilioni ya Mayahudi katika Vita vya Pili vya Dunia.
Uamuzi huo wa Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani umepingwa vikali na jamii ya Wayahudi wachache nchini Italia na makuhani wenye misimamo mikali wa Kiyahudi. Mayahudi hao wamesema kwamba hatua ya Papa inatambuliwa kuwa ni sawa na Vatican kukana mauaji ya holocaust.
Kiongozi wa Mayahudi wa Italia Renzo Gattegna amemtaka Papa Benedict XVI kutoa taarifa rasmi akieleza msimamo wake kuhusu "holocaust" na madai ya kuuawa Mayahudi milioni sita katika Vita vya Pili vya Dunia. 355812
captcha