Shirika rasmi la habari la Imarati (WAM) limeripoti kuwa, mkutano huo unafanyika kwa nara ya "Elimu Nafsi ya Jadi" ukisimamiwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Wataalamu wa Elimu Nafsi wa Kiislamu.
Mada kuu zinazojadiliwa katika mkutano huo ni "elimu nafsi katika mtazamo wa Kiislamu, njia za kuifanya elimu nafsi kuwa ya kienyeji na uzinduzi wa nyanja mpya katika medani ya elimu nafsi katika vyuo vikuu vya ulimwenu wa Kiislamu.
Wataalamu wa saikolojia na wahadhiri wa vyuo vikuu kutoka nchi za Iran, Saudi Arabia, Pakistan, Iraq, Indonesia, Palestina, Jordan, Malaysia, Australia, Uingereza, Misri, Sudan, Imarati, Kuwait na Aljeria wanashiriki katika mkutamno huo wa siku mbili.
Makao makuu ya Jumuiya ya Kimataifa ya Wanasaikolojia wa Kiislamu iko katika mji mkuu wa Sudan Khartoum.
Jumuiya hiyo ina wanachama kutoka nchi mbalimbali za Kiislamu. 358040