Gazeti la nchi hiyo la Akhbar al-Khaleej, limemnukuu Muhammad Ibrahim, Mkurugenzi Mwandamizi wa benki hiyo akisema kuwa, benki hiyo ya Bahrain imefanikiwa kupata zawadi hiyo baada ya uamuzi wa mwisho wa timu ya marefa wa jarida la Ulimwengu wa Uchumi ambalo wanachama wake ni waandishi mashuhuri wa kimataifa kuhusiana na masuala ya uchumi na pia washauri wa kiuchumi wa dunia. Wanachama wengine wa jarida hilo ni wakuu wa benki na wataalamu wa masuala ya sarafu.
Amesema, masuala mengine yaliyoifanikisha benki hiyo kutunukiwa zawadi ni ubora wa huduma zake pamoja na muamala mzuri kwa wateja wake.
Muhammad Ibrahim amesisitiza kwamba, zawadi hiyo ni muhimu mno kwa benki hiyo na kwamba itaongeza maradufu juhudi za viongozi wake za kutaka kuimarisha daima huduma na shughuli zinazofanyika katika benki hiyo.
Amesema zawadi hiyo itawapa moyo zaidi wafanyakazi na wasimamizi wa benki hiyo kuhisi kuwa na majukumu mazito zaidi ya kuwahudumia vyema wateja wake na kuwavutia wengine wengi ambao sasa si wateja wa benki hiyo. 360143