IQNA

Mafunzo ya muda kuhusu dini ya Kiislamu kutolewa katika Chuo Kikuu cha jimbo la Tennessee, Marekani

10:44 - February 07, 2009
Habari ID: 1741066
Mafunzo ya muda kuhusu dini ya Kiislamu yataanza kutolewa tarehe 14 Februari katika Chuo Kikuu cha Vanderbilt kwenye jimbo la Tennessee nchini Marekani.
Kituo cha habari cha Insidevandy kimeripoti kuwa mafunzo hayo ya muda kuhusu Uislamu yatasimamiwa na "Kituo cha Mafunzo ya Kiislamu cha Zeitun", "Ofisi ya Kueneza Maisha ya Kidini" na "Umoja wa Wanachuo wa Kiislamu". Mafunzo hayo yamekusanywa kutoka kwenye vitabu mashuhuri ya Kiislamu.
Lengo la kutolewa mafunzo hayo ni kukidhi haja ya watu wa eneo hilo ya kutaka kujua misingi ya dini ya Kiislamu na kukabiliana na propaganda chafu zinazotolewa na vyombo vya habari dhidi ya dini hiyo.
Mafunzo hayo yatatolewa na Sheikh Ghiyathi Makenzi aliyehitimu katika chuo cha mafunzo ya Kiislamu cha Madina.
Masomo ya muda kuhusu dini ya Kiislamu yamekuwa yakitolewa kila mwaka tangu mwaka 2000 katika eneo hilo baada ya kupokelewa kwa wingi na wananchi. 360248

captcha