IQNA

Sisitizo la al-Azhar na Kanisa la Anglican la kuunga mkono mazungumzo ya dini

10:37 - February 09, 2009
Habari ID: 1741981
Muhammad Sayyid Tantawi, Sheikh wa al-Azhar na Rowan Williams, Kiongozi wa Kanisa la Anglican na Askofu Mkuu wa Canterbury nchini Uingereza wamesisitiza uungaji mkono wao juu ya kufanyika mazungumzo ya dini mbalimbali.
Gazeti la al-Watan la Saudi Arabia limesema kuhusiana na suala hilo kwamba, viongozi hao wawili wa kidini wamesema kwamba lengo lao la kuunga mkono juhudi zinazofanyika kwa lengo la kufanikisha mazungumzo hayo, ni kufikia shahaba ya wafuasi wa dini mbalimbali duniani kuishi pamoja kwa amani. Aidha wamesisitiza kwamba kuenezwa moyo wa ushirikiano na kusameheana, kupambana na ugaidi kutambuliwa uhuru wa kujieleza na haki za kiraia za wafuasi wa dini tofauti ni malengo mengine yanayofuatiliwa na mazungumzo hayo.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika mjini Cairo, Tantawi amesisitiza juu ya kuwepo ushirikiano wa al-Azhar na Kanisa la Anglican kwa madhumuni ya kuimarisha nafasi za viongozi wa kidini ili kuwawezesha kukabiliana na vitendo vya watu wenye misimamo ya kupindukia mipaka, kusambazwa thamani za kidini kama vile usamehevu na kuondoa athari mbaya za mgogoro wa kifedha duniani.
Rowan Williams yuko mjini Cairo Misri kwa lengo la kufanya mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano na viongozi wa al Azhar.361231
captcha