Gazeti la nchi hiyo la ar-Riyadh limesema kuwa wasomi wa Qur'ani pamoja na wataalamu wa taaluma ya habari watashiriki katika semina hiyo.
Muhammad Salim bin Shadid al-Aufi, mkuu wa kamati inayoandaa semina hiyo amesema kuwa semina hiyo imeandaliwa katika kivuli cha malengo ya Jumuiya ya Mfalme Fahd ya kueneza mafundisho ya Qur'ani na kumhudumia Mwenyezi Mungu.
Kamati inayoandaa semina hiyo pia imezindua mtandao chini ya anwani www.Quranlt.orq kwa lengo la kuwawezesha watafiti na wanafikra walio na hamu ya kushiriki katika semina hiyo kujua masharti, maudhui na mambo yatakayojadiliwa katika semina hiyo.
Al-Aufi amesema kuwa malengo ya semina hiyo ni pamoja na kusisitiza juu ya umuhimu wa teknolojia na taaluma ya habari katika kujifunza na kueneza mafundisho ya Qur'ani, kubainisha njia za kufikiwa malengo ya Qur'ani, kutathmini utendaji wa tovuti na kanali zinazojishughulisha na masuala ya Qur'ani, kuchunguza ratiba zinazosaidia mafunzo ya Qur'ani na kutoa tahadhari kuhusiana na mipango pamoja na njama za kupinga kitabu kitakatifu cha Waislamu. 367026