IQNA

Mashindano ya Qur'ani na haditi za Mtume ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Oman

11:00 - March 02, 2009
Habari ID: 1750420
Mashindano ya kusoma Qur'ani na hadithi za Mtume Muhammad (saw) yamepangwa kufanyika tarehe tano mwezi huu wa Machi nhini Oman.
Gazeti la Shabiba la Oman limeandika kuwa mashindano hayo ya siku mbili yanasimamiwa na ofisi inayoshughulikia masuala ya wanafunzi wa vyuo vikuu katika maeneo mbalimbali ya Oman.
Washiriki katika mashindano hayo wanatakiwa kuwa wamehifadhi juzuu za 9, 10, 11, 12 za Qur'ani Tukufu na haditi 30 za Mtume (saw) na kuwa na uwezo wa kuzitolea sherhe na ufafanuzi.
Miongoni mwa malengo ya mashindano hayo ni kuzidisha maarifa ya Qur'ani ya wanafunzi wa vyuo vikuu na kueneza moyo wa ushindani sahihi kati yao.
Washiriki katika mashindano hayo walishinda mashindano ya awali ndani ya vyuo vikuu na kufanikiwa kuingia duru ya mwisho itakayofanyika Alkhamisi ijayo. 370811

captcha