IQNA

Jarida la Qur'ani la Kashila lachapishwa kwa lugha ya Shqip

11:24 - April 05, 2009
Habari ID: 1760376
Toleo la 34 la jarida la masuala ya Qur'ani la Kashila kwa maana ya "Mawaidha" ambalo linajadili maisha ya Nabii Muhammad (saw) limechapishwa nchini Albania kwa lugha ya Shqip.
Jarida hilo ni moja ya bidhaa za kiutamaduni za Jumuiya ya Qur'ani ya Albania ambazo zinatolewa kwa ajili ya wananchi zikijadili masuala ya Qur'ani na dini.
Sehemu ya kwanza ya toleo la sasa la jarida hilo inajadili uhusiano wa mwanadamu na ulimwengu wa kiroho na kufafanua kwamba Mitume ndio daraja la mawasiliano kati ya ulimwengu na Mwenyezi Mungu Muumba.
Sehemu ya pili ya jarida hilo inajadili masuala na maudhui mbalimbali kama vile, Qur'ani kitabu cha hekima, aya za Qur'ani kuhusu Mtume Muhammad (saw), kumpenda Mtume Muhammad (saw) na kadhalika.
Sehemu nyingine ya jarida la Kialbania la Kashila ambayo imebeba anwani: Je, unajua? inazungumzia masuala ya siku ya Kiyama katika Qur'ani, awamu za kuumbwa mwanadamu, kifo na vazi la hijabu ya Kiislamu. 382046




captcha