Hujjatul Islam Mujtaba Kalbasi amesisitiza kuwa ushindi wa harakati za mapambano umetokana na imani ya wanamapambano na utiifu wao kwa faqihi mtawala. Sheikh Kalbasi amesema kuwa faqihi mtawala ambaye ni mujtahidi aliyekamilisha masharti katika zama za kughibu Imam wa zama, huwa kiunganishi kati ya Imam maasumu na umma wa Kiislamu.
Amesema kuwa baada ya kufariki dunia Mtume Muhammad (saw) wadhifa wa kuongoza umma ulihamia kwa maimamu katika kizazi cha mtukufu huyo na kwamba kwa sasa ambapo Imam wa Zama amekwenda ghaibu, faqihi mtawala ndiye anayechukua jukumu la kuongoza umma wa Kiislamu.
Mkurugenzi wa Kituo cha Imam Mahdi (as) amesisitiza kuwa itikadi ya mwokozi wa aheri zamani huzidisha moyo wa kupigania uhuru na kupambana na dhulma na kwamba mfano wa suala hilo ni ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran chini ya uongozi wa hayati Imam Khomeini, harakati ya Hizbullah ya Lebanon na mapambano ya Kiislamu ya Gaza. 382582