IQNA

Kitabu kipya kuhusu Uislamu chachapishwa nchini New Zealand

12:37 - April 16, 2009
Habari ID: 1765623
Kitabu kipya kilichopewa anwani ya 'New Zealand kwa Ajili ya Waislamu' ambacho kinachambua masuala mbalimbali kuhusiana na jinsi Uislamu ulivyoingia nchini humo kimechapishwa na kusambazwa kote nchini humo.
Kwa mijibu wa Indiannewslink, kitabu hicho kinafafanua hali ya Waislamu wa New Zealand, misikiti na vituo vya Kiislamu, uchinjaji wa Kiislamu, maduka ya nyama halali na pia nyakati mbalimbali za kuadhiniwa katika miji tofauti ya nchi hiyo.
Kitabu hicho pia kinafanya juhudi za kurekebishwa sura ya Uislamu iliyopotoshwa na maadui nchini humo na kuwafanya raia wa nchi hiyo waweze kupata sura halisi ya dini hii tukufu. Kitabu hicho kilicho na kurasa 75 kimechapishwa na Taasisi ya Chapa ya Kiislamu ya New Zealand iliyoko katika mji wa Auckland. 388796
captcha